HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2019

MASHINDANO YA BAMMATA SOKA JKT WAAGA KWA KISHINDO

Wachezaji wa timu ya Mpira ya Wavu ya Magereza na JKT wakichuana katika michuano ya Majeshi BAMMATA jijini Dar es Salaam. Magereza walishinda Seti 3-1. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).


Nahodha wa Kanda ya Magereza Sajini Tausi Abdul  akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa mchezo wa mpira wa kikapu katika michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika mchezo huo Ngome ilishinda Magereza  vikapu 68 kwa 60.


 
Na Luteni Selemani Semunyu

Mashindano ya Majeshi Tanzania BAMMATA yameendelea kushika kasi huku timu ya Soka ya JKT ikiaga mashindano hayo kwa mwaka 2019 kwa kishindo baada ya kuifunga Zimamoto magoli 10 kwa Moja.

Matokeo hayo yamejitokeza katika mchezo wa kufunga Dimba uliochezwa katika Dimba la Uhuru licha ya Timu hizo zote hazikuwa na nafasi ya kuingia katika Hatua ya Nusu Fainali.

Katika Soka sasa Mchezo kati ya Ngome na Magereza unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Dimba la Uhuru utaamua nani wa kucheza na Polisi na nani kucheza na SMZ katika hatua ya Nusu Fainali.

Katika Ridha atika mchezo mwingine  Mpira wa Kikapu  Wanawake mchezo uliokuwa ukiamua mcshindi wa Pili Ngome wameibuka na Ushindi kwa Vikapu 68 kwa 60.
Katika Mpira wa Wavu   wanawake Magereza wameifunga JKT kwa seti tatu kwa Moja huku kwa Upande wa Wanaume  Ngome wameifunga  Polisi Seti tatu bila.

Katika Shabaha pistor wanawake mshindi wa Kwanza Pc Pili Mkama wa pili PC Salvina Mhiche na PC Bertha Jonathan wote wa Polisi.

Kwa Upande wa Wanaume Sajini Kenya Kiula wa Polisi wa pili ni Sajini Jumanne Wambura wa Ngome na watatu ni PC Joseph Mwenda Polisi. 

Kwa Upande wa Rifle  Wanawake ni Private Elizabeth Kibondo Ngome wa pili ni  Mteule Daraja la Pili Sophia Ramadhani wa Ngome na PC Sharifa Kibwana Ally wa Polisi huku kwenye Riadha relay wanaume Mita 400 Timu ya Ngome imeibuka na Ushindi.

No comments:

Post a Comment

Pages