Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Windlab Limited imetangaza makubaliano ya uwekezaji wa kiasi cha dola za kimarekani
10,000,000 na kampuni ya Eurus Energy Holdings Corporation (Eurus) katika
miradi ya kibiashara ya Windlab East Africa.
Windlab East Africa (WEA) inamiliki rasilimali za maendeleo ya
miradi iliyopo katika kampuni hiyo pamoja na haki ya kutekeleza miradi ijayo
katika nchi za Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi na Malawi.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kampuni
hiyo, Rasilimali za Windlab za Afrika Mashariki kwa sasa zinahusisha miradi ya
maendeleo iliyoko katika mkakati ya utekelezaji yenye jumla ya takribani
1,650MW ya uwezo unaotarajiwa, ambayo iko katika ngazi ya awali mpaka ngazi ya
miradi iliyoidhinishwa.
“Mradi wa 300MW wa Miombo Hewani Wind Farm nchini Tanzania, ambao
umeorodheshwa katika orodha ya miradi inayofadhiliwa na serikali.
Nchini Kenya,
kampuni ya Windlab imeingia katika ushirikiano na serikali ya Mkoa wa Meru
katika uendelezaji wa mradi wa nishati ya muunganiko ambao unajumuisha upepo,
Jua,na uhifadhi kwa njia ya betri mpaka kufikia uzalishaji wa 166MW chini ya
mpango wa PPP.
''Windlab itatumia fedha hizi kuongeza kasi ya maendeleo ya miradi
ya msingi Afrika Mashariki kukidhi mahitaji makubwa ya umeme ambayo
hayajafikiwa. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Idadi ya watu walioko kusini mwa
Jangwa la Sahara Afrika kwa sasa inazidi watu 1 billioni na wanafurahia ukuaji
wa kasi wa uchumi (GDP) duniani; Ethiopia asilimia 8.2%, Kenya asilimia 5.5%,
na Tanzania asilimia 6.8%,”
Hata hivyo upatikanaji wa nishati ya umeme na uwezo wa uzalishaji
wa nishati hiyo umebakia kuwa wa kiwango cha chini; kwa mfano, Tanzania ina
idadi ya watu wapatao 59 millioni lakini ina kiasi cha 1,600MW cha uzalishaji
wa nishati.
“Tunafuraha sana kupata
uungwaji mkono wa kampuni ya Eurus kama wadau katika WEA. Tutafanya kazi kwa
pamoja kuharakisha maendeleo ya miradi yetu katika kanda hii.
Wakati sehemu
kubwa ya masoko haya hayakosi changamoto, mahitaji ya uwekezaji mkubwa katika
miundombinu ya uzalishaji wa umeme uko wazi.” Alisema bwana Roger Price,
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Windlab.
No comments:
Post a Comment