MKUU wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda, amepokea kiasi cha Sh. Mil. 20 kutoka kwa
Balozi wa Falme za Kiarabu na wamiliki wa Erminet Khalifa AbdulRahman
Al-Marzooqi wamejitolea kuwasomesha wanafunzi wa kike 100 wa shule yoyote na
mkoa wowote ule ili kuchangia elimu kwa wanafunzi ambao wamefahulu vizuri kidato
cha nne na kukosa ada ya kuendelea masomo.
Ambapo Mh. Makonda
ameomba fedha hizo zielekezwe kwa wanafunzi wakike waliofanya vizuri katika
mtihani wa kidato cha nne kwenye masomo ya Sayansi na kushindwa kuendelea
kidato cha tano kwa kukosa ada.
Kwa upande wake Balozi
alishukuru kwa ulafiki uliokuwepo baina ya nchi yao na Tanzania na kusema
uendelee Kudumu.
"Namshukuru mkuu
wa mkoa na nimpongeze kwa Maendeleo anayoendelea kufanya katika na kuwa na
muungano mzuri wa nchi zetu tutaendelea kutoa ushirikiano katika maendeleo ya
elimu pamoja na jamii yote nikujenga urafiki bora na imara " alisema
Khalifa AbdulRahman.
"Hizi fedha
zitumike kuwa somesha wanafunzi wenye hali ngumu ya maisha nasi tofauti na
hapo, kila wilaya watatoa wanafunzi 20 wa kike ambao wamefanya vizuri katika
mtihani wa kidato cha nne kwenye masomo ya Sanyansi ambao awana uwezo wa kupata
ada ya kuendelea na masomo wapewe nafasi hizo hata kama ni mtoto wa mvuvi au Yatima
au anahali ngumu ya maisha apate nafasi ya kusomeshwa popote bila kuangalia
kitu chochote awe amefahuru vizuri wawe na wazazi au hanao ila anahali ngumu ya
maisha"anasema Makonda.
Aidha Makonda
amemuomba Balozi huyo kutujengea uwanja wa mpira wa kimataifa utakaoingia watu
kuanzia 1000 na kuendele wenye hadhi ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment