Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Abella Tarimo,
akichangia mada katika mjadala ulioandaliwa na benki hiyo kuadhimisha
Siku ya Mama Duniani. Pamoja nae ni Meneja Uhusiano Mwandamizi, Amana na
Biashara wa NMB, Beatrice Mwambije (kulia) na Meneja Mikopo
Chechefu-Pauline Mohele.
Walitoa msaada kwa Kituo cha Afya cha Buzuruga Mwanza.
NMB MT. Uluguru.
NMB Mwanjelwa.
NMB Mzengo.
Na Mwandishi Wetu
WANAWAKE nchini wameshauriwa
kutokata tamaa kufanyia kazi taaluma walizonazo huku wakizihudumia familia zao
kwa mujibu wa majukumu yao nyumbani.
Ushauri huo umetolewa jijini
Dar es Salaam Mei 12, 2019 na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Abella
Tarimo katika mjadaLa ulioandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Mama
Duniani (Mother's Day).
Alisema ili wanawake waweze
kufanikiwa katika jambo lolote juhudi na uwazi juu ya suala wanalolifanya
zinahitajika.
"Ili mradi mtu uwe na nia na
unaungwa mkono huku ukiweka jitihada za dhati bila kusahau familia yako,
utafanikiwa. Wapo baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakijikwamisha kwa kudhani
kuwa hawawezi kufanyia kazi ujuzi waliousomea na kufanikiwa huku wakizihudumia
familia zao ipasavyo, jambo ambalo si sawa," alisema Bi. Tarimo.
Alisema kwa kuanzia mafanikio
wanawake wafanyakazi hawana budi kujenga utamaduni wa kushirikiana pamoja na
kuungana mkono bila kuathiri majukumu yao kifamilia.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano
Mwandamizi, Amana na Biashara wa NMB, Beatrice Mwambije akichangia mada katika
mjadala huo, aliwataka akina mama ambao wako kazini na wamekata tamaa na hata
kufikiria kuacha kazi ili wakalee familia zao kutathmini mara mbilimbili kabla
ya kufanya maamuzi yao.
"Ni kweli ukiangalia
majukumu ya mama mwenye mtoto mchanga anaweza kubanwa akashindwa kutekeleza
kazi zake ofisini...lakini hiki kisiwe kikwazo kuna namna unaweza kujipanga na
kukabiliana na yote hayo na ukaendelea na kazi pasipo kuathiri pande
zote," alisema Bi. Mwambije.
Aidha aliwataka akinamama
kuangalia usalama wa familia na watoto kwa maisha ya baadaye wanapokuwa wakubwa
hivyo kuna kila sababu ya kuwajengea msingi imara.
Mjadala huo ulioandaliwa na
Benki ya NMB ulienda sambamba na maadhimisho ya 'Siku ya Mama Duniani’ huku ukisisitiza kutambuliwa kwa majukumu ya
kinamama duniani kote kwani wanamchango mkubwa kimaendeleo.
Benki ya NMB imeadhimisha siku
hii kwa kualika wadau mbalimbali kujadili mada ya mama katika matawi yake yote
nchi nzima pamoja na baadhi yao kutoa misaada kwa watoto na akina mama.
#Nani kama Mama
No comments:
Post a Comment