Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda wakigawa zawadi kwa watoto wanaoelelewa katika kituo ha watoto yatima cha Maunga nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada ya kujumuika pamoja nao katika sikukuu ya Eid-El Fitr.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda wakila pamoja na watoto wanaoelelewa katika kituo ha watoto yatima cha Maunga nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada ya kujumuika pamoja nao katika sikukuu ya Eid-El Fitr.
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda akizungumza na watoto wanaoelelewa
katika kituo ha watoto yatima cha Maunga nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam
juzi baada ya kujumuika pamoja nao katika sikukuu ya Eid-El Fitr.
Na Mwandishi Wetu
MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amesheherekea sikukuu ya Eid-El Fitr kwa kujumuika na watoto yatima wanaoelelea katika kituo cha Maunga, kilichopo Hananasif Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mwenda
aliungana na watoto hao kwa kujumuika katika chakula cha mchana
alichokuwa amekiandaa yeye na familia yake nyumbani kwake eneo la
Mikocheni na kuwataka watoto hao kutia mkazo katika masomo ili waweze
kuja kulitumikia Taifa hapo baadae.
Akizungumza
na watoto hao, Mwenda aliwataka kutojiona kama wametengwa na kwamba
jamii ipo pamoja nao wakati wote hivyo suala la msingi kwao ni kuendelea
kuwa watoto wema kwa kumcha Mungu wakati wote bila kusahau kuwaombea
dua wale wote wanaowalea na kuwakumbukuka kwa namna mbalimbali.
“Tieni
mkazo katika masomo yenu wakati wote mnapokuwa shuleni na hata
nyumbani, kumbukeni kuwa elimu ndio urithi wenu mkubwa zaidi ya kitu
kingine chochote, mkumbuke pia kusali na kuwaombea njema kwa Mungu wale
wote wanaowakumbuka” alisema Mwenda.
Kwa
upande wao watoto hao, walimshukuru Mwenda kwa hatua yake ya kuwa
pamoja nao siku hiyo na kumtaka kuendelea kufanya hivyo wakati mwingine
anapojaliwa uwezo.
Walisema
kitendo cha Mwenda kujumuika nao amekuwa akikifanya kila mwaka huku
wakiwaomba watu wengine wenye uwezo kuiga kitendo cha Meya huyo mstaafu
kwani kinawafanya wasijikie faraja na kujiona kama watoto wengine
wanaolelewa na wazazi wao.
Mbali
na vyakula na burudani mbalimbali yakiwemo mashindano ya kuimba
kucheza, watoto hao pia walizawadiwa zawadi mbalimbali yakiwemo
madaftari, mabegi ya shule jambo lililowafanya watoto hao kufurahia.
No comments:
Post a Comment