Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Abubakar Zuberi Bin 
Ally, Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania wakati alipowasili kwenye uwanja 
wa ndege wa Tanga kushiriki katika Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Tanga 
Beach Reort jijini Tanga, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Baadhi ya  Viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati 
alipohutubia Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach 
Resort  jijini Tanga, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye ukumbu wa 
Hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi 
ya Waziri Mkuu)
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye ukumbu wa 
Hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi 
ya Waziri Mkuu).
Tanga, Tanzania 
WAZIRI
 MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu kote nchini waendeleze 
utulivu, amani na uadilifu waliouonesha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu
 wa Ramadhani kwani kwa kufanya hivyo, watasaidia kukuza umoja wa 
kitaifa, uchumi na kuboresha huduma za jamii.
Amesema
 ni vema wakatambua kwamba uadilifu waliouonesha ndani ya Mwezi Mtukufu 
wa Ramadhani ni silaha muhimu hususan katika kuimarisha maendeleo na 
kudumisha haki, umoja, usawa, upendo na utulivu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Juni 5, 2019)kwenye Baraza la Eid El Fitri, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Tanga Beach Resort jijini Tanga.“Nawashi sana kuyaenzi mema yote mliyoyafanya kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan’’.
Kadhalika,
 Waziri Mkuu amezipongeza taasisi za Kiislamu na imani nyingine ambazo 
zimejenga shule ili kuchangia maendeleo ya elimu kitaifa lakini 
amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza shule nyingine na vyuo zaidi
 pamoja na kuziboresha zile zilizopo ili kusaidia jitihada za Serikali 
katika kuboresha huduma za jamii nchini
Amesema
 licha ya juhudi inazozichukua, Serikali peke yake haina uwezo wa 
kueneza huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji katika kila pembe 
ya nchi hivyo, inapotokea taasisi za Kiislamu au madhehebu mengine 
yakaweka mikakati ya kueneza huduma hizo, basi bila shaka Serikali ipo 
tayari kuunga mkono juhudi hizo na kuchangia ufanisi wake. 
Wakati huo huo,
 ameitaka BAKWATA ichukue hatua za makusudi katika kuhakikisha huduma 
nyingi za maendeleo na za kijamii zinaifikia kwenye mikoa mingi zaidi ya
 pembezoni. “Huu ni wakati muafaka sasa wa kutafakari ni namna gani 
Watanzania wa maeneo mengine nao watanufaika na uwepo wa huduma 
mbalimbali kama vile elimu, afya na nyinginezo.“
Kwa upande wake,Mufti
 na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally ametumia 
fursa hiyo kuwataka waislam wote nchini wabadilike na waache mazoea ili 
waweze kusonga mbele kielimu na kiuchumi.
Sheikh
 Zubeir amesema ni vema kwa waislamu wakajiimarisha kiuchumi kwa sababu 
kutawaondolea changamoto za kuendesha shughuli zao mbalimbali na hivyo 
watakuwa wamejiletea maendeleo na kuboresha maisha yao.
Mbali
 na wito huo pia amewataka waislamu wote wahakikishe wanatii 
mamlaka yaliyo juu yao , viongozi waliopo madarakani wawe wa kiserikali 
na wa kidini kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu
Kwa
 upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athuman amesema ili nchi iweze kuendelea kuwa na 
amani,  utulivu na usalama watanzania wote hawana budi kuungana pamoja 
katika kupiga vita vitendo vya rushwa.
"Rushwa
 ni dhambi kubwa na hukumu yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni moto kwa 
sababu rushwa ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo, hivyo tuungane 
pamoja kupinga rushwa ndani ya nchi yetu kama Rais Dkt. John Magufuli 
anavyotuongoza."
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment