Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime.
Dar es Salaam, Tanzania
Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kuwashukuru
wananchi wote kwa jinsi wanavyoendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa na ufadhili unaowezesha
kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu nchini kwani uhalifu unaendelea
kupungua na kuifanya nchi yetu kuendelea
kuwa shwari na salama.
Yapo
matukio mchache ambayo tunaomba ushirikiano zaidi kutoka kwa wananchi
wote katika kupeana elimu ya kuyaepuka kuyatenda matukio kama vile mauaji
yanayotokana na vitendo vya wananchi kujikulia
sheria mikononi, wivu wa mapenzi na
ulevi. Pia matukio ya ubakaji na
ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva.
Jeshi la Polisi Tanzania lina amini kama kila
mtu kwa nafasi yake akishiriki katika kutoa
elimu, kuonya na kufiwachua wanaotenda uhalifu huo, kuanzia ngazi ya familia matukio
ya aina hiyo yatapungua kwa kiasi kikubwa.
Mtakumbuka pia tarehe 01/06/2019 serikali ilitoa
maelekezo kuwa, ndiyo mwisho wa matumizi
ya mifuko ya plastiki hapa nchini na utekelezaji ukaanza kwa ufanisi mkubwa. Jeshi la Polisi linatoa wito agizo hilo
liendelee kuzingatiwa na wenye mifuko ya aina hiyo waisalimishe kama
ilivyoelekezwa na kama kuna mwenye taarifa za mtu mwenye kumiliki mifuko hiyo
atoe taarifa Polisi au mamlaka zingine ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria
na kanuni ziweze kuchukuliwa.
Aidha, kama
mnavyofahamu tunaelekea kipindi cha sikukuu ya Eid El Fitri ambayo
husheherekewa duniani kote baada ya
mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watanzania
wote kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama ili waweze kusheherekea
kwa amani na utulivu sikukuu hiyo kubwa na muhimu.
Kila mmoja
ajiepushe na vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama wa maisha na mali zao kama vile kuacha
nyumba bila waangalizi, ulevi wa kupindukia, kuruhusu vijana na watoto walio
chini ya uangalizi wa wazazi kwenda katika nyumba za starehe au maeneo
yanayoweza kuhatarisha usalama na utu wao. Kujiepusha kuendesha vyombo vya moto
bila kufuata sheria za usalama barabarani kama vile kuendesha chombo cha moto
ukiwa umelewa , mwendo kasi, pamoja na kujaza abiria kupita kiasi.
Pamoja na kwamba, Jeshi la Polisi katika Mikoa yote limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya ibada na maeneo mengine ambayo yatakayokuwa na
mikusanyiko mikubwa ya watu tunaelekeza kila mmoja usalama uanzie kwake na kwa wale wanaomiliki maeneo ya starehe
wazingatie maelekezo ya kiusalama waliopewa na
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi na watakayoendelea kuwapa.
Pia tunatoa onyo kwa wale wanaodhani wanaweza
kutumia sherehe hizi kufanya uhalifu watambue kuwa watashughulikiwa kwa nguvu zote
kwa mujibu wa sheria za nchi.
Tunawaomba wananchi
wote pale watakapoona viashiria au kumtilia mtu mashaka kuwa huenda akawa mhalifu watoe taarifa kupitia namba za simu za bure 0787 668 306 au 111 au 112.
No comments:
Post a Comment