June 13, 2019

Waliohukumiwa maisha kwa kosa la kuchoma kituo cha Polisi moto, wakata rufaa

Washtakiwa waliochoma kituo cha Polisi wakiingia mahakamani
Wakili wa warufani Prof. Abdallah Safari, akizungumza na ndugu wa warufani hao nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
 
Na Janeth Jovin

RUFAA dhidi ya washtakiwa watatu kati ya wanane waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi bunju imeshindwa kuanza kusikilizwa kufuatia majalada ya warufani hao kuchanganywa.
 
Hali hiyo imetokea leo Juni 13,2019  baada ya wakili wa Serikali, Sadah Mohamed kuieleza mbele ya Naibu msajili wa Mahakama Kuu, Crisencia Kisongo kuwa, rufaa hiyo leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mwenendo wa kesi (proceedings) alionao siyo za mrufani aliyekuwa mahakamani hapo, bali anayo ya mrufani Abrahamu Minga.

Alidai wanaomba muongozo wa mahakama ili kufahamu nini kifanyike, rufaa iliyoko mbele yako ni ya mrufani Konzo ambayo hajaipata na si ya mrufani Minga aliyonayo.

Wakili wa warufani hao Profesa Abdallah Safari alidai kuwa samasi (hati ya wito) aliyonayo yeye ni ya washtakiwa watatu ambao ni, Yusuph Sungu maarufu kama Mayuku ambae leo hakuwepo mahakamani, Juma Konzo na Abrahamu Minga ambapo maelekezo ya warufani hao.

Baada ya maelezo hayo rufani hiyo imeahirishwa hadi Juni 17,2019

Februari 23, mwaka huu,  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia wakili wake Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwahukumu kifungo cha maisha washtakiwa wanane baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A ambapo 10 waliachiwa huru.

Waliohukumiwa ni Yusuph Sugu (40), Juma Kozo (32), Rashid Liwima (29), Baraka Nkoko (23), Abuu Issa (36), Abraham Mninga (23), Veronica Ephraem (32) na Ramadhan Said (22).

Walioachiwa huru ni Mrisho Majaliwa (30), Hamis Ndege (37), Seleman Gwae (33), Menge’nya Anthony (28), Rehema Hussein (32) Rajabu Ally (25), Ally Athuman (24), Amina Matipwili (33), Gubila Temba (51) na Mariam Honza (44).

Walikuwa wanakabiliwa na makosa sita likiwamo la kuchoma kituo hicho moto ambapo wanadaiwa Julai 10, 2015. Walichoma kituo cha polisi ambacho ni mali ya umma jambo ambalo ni kosa la kisheria.

No comments:

Post a Comment

Pages