Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt.
Naftali Ng’ondi akizungumza na viongozi wa dini wakati wa kikao baina ya Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kikao cha
kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya
Familia kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW).
Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Jinsi ya kiume imetajwa kuwa ni moja kati ya
watendaji wakubwa wa vitendo vingi vya ukatili dhidi ya Mwanamke na Mtoto
katika jamii ambavyo vimekuwa vikiathiri malezi ya watoto na ustawi wa familia.
Hayo yamebainika leo jijini Dar es Salaam katika
kikao katika ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na
Viongozi wa dini katika kujengewa uelewa kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya
Familia.
Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Katibu
Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu, Kamishna wa
Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa kwa mujibu wa Utafiti wa hali
ya ukatili dhidi ya watoto uliofanyika na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na UNICEF wa mwaka 2011 unaonesha kuwa
mtoto 1 kati ya watoto 3 wa kike na 1 kati ya 7 wa kiume walifanyiwa vitendo
vya ukatili kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
Dkt. Ng’ondi ameongeza kuwa asilimia 72 ya
wasichana na asilimia 71 ya wavulana walifanyiwa ukatili wa kimwili na vilevile
robo ya watoto walifanyiwa ukatili wa kiakili.
“Uandaji wa Ajenda hii umetokana na hali halisi ya
ongezeko la changamoto zinazomkabili mtoto hasa zinzaoanzia katika ngazi ya
familia” alisema
Kamishna Ng’ondi ameeleza kuwa vitendo vya ukatili
pia vimekuwa vikisababishwa na ongezeko la migogoro ya ndoa ambapo imesababisha
watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili ambapo amesema kwa mwaka kwa mujibu
wa takwimu za Ofisi ya Ustawi wa Jamii inaonesha kwa muda wa miezi tisa kuanzia
Julai, 2018 hadi Marchi 2019 jumla ya mashauri ya ndoa 16,832 ukilinganisha na
mashauri 13,382 kwa mwaka 2017/2018.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Manendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bi. Mwajuma Magwiza ameeleza kuwa jamii ya kitanzania inakumbwa na
changamoto nyingi zikiwemo ukatili dhidi ya wanawake na watoto na Serikali
imekuwa ikiandaa mikakati mbalimbali katika kukabiliana na changamoto hzio ikiwemo
Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi/Walezi katika malezi na matunzo ya
familia.
Naye Mwakilishi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania
(BAKWATA) Sheikh Hassan Said Chizenga amesema kuwa Ajenga hii inatakiwa kushirikisha
Sekta nyingine kama vile utamaduni na michezo ili iweke misingi bora katika
kujenga maadili ya watoto wetu katika malezi na makuzi yao.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Jamii kutoka Baraza
la Maaskofu Tanzania (TEC) John Riziki amesema kuwa Baraza hilo limejidhatiti katika
kuhakikisha wanasaidia na wazazi/walezi katika malezi kwa kufanya somo la dini
kufundishwa katika shule za Msingi na Sekondari ili kuhakikisha watoto wanakuwa
katika maadili mema.
Kikao hiki cha kuwajengea uelewa viongozi wa dini
kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya
Familia ambayo kinakuja mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(Mb) katika
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika mkoani Geita Juni, 16.
No comments:
Post a Comment