July 11, 2019

Magnet, St. Patrick kuiwakilisha Tanzania Norway, Sweden

Mwenyekiti wa Kituo cha Magnet Youth Sports, Tuntufye Mwambusi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu timu nne zitakazokwenda Norway na Sweden kushiriki mashindano ya vijana wenye miaka 11, 12 na 15 yatakayofanyika Julai 14-21. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cornel Barnabas na kulia ni Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo. (Picha na Francis Dande).

 
TIMU nne za kituo cha Magnet Youth Sports, zinatarajia kuiwakilisha Tanzania katika michezo inayotarajia kuchezwa katika nchi za Norway na Sweden.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kituo hicho, Tuntufye Mwambusi, mashindano hayo yanatarajia kuanza Julai 14-21 yakishirikisha vijana wenye miaka 11, 12 na 15.
Mwambusi, alisema katika mashindano hayo, kituo hicho kitaungana na Sekondari ya St. Patrick ya jijini Dar es Salaam.
“Tunakwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo, ambayo yanakuwa na timu hadi 3,000, tutafanya vizuri katika mashindano hayo,” alisema Mwambusi.
Alitumia fursa hiyo, kuwaomba wadau na serikali kuboresha zaidi michezo kwa kukuza na kuendeleza vijana, ambao ndio tegemeo la timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cornel Barnabas, alisema hivi sasa mkazo wao wameuelekeza zaidi kwenye soka la vijana, ambalo ndio nguzo ya michezo.

No comments:

Post a Comment

Pages