July 11, 2019

SERIKALI YAIAGIZA MUHIMBILI KUFANYA UTAFITI WA MAGONJWA YANAYOSAMBAZWA NA MBU

Naibu  Waziri wa Afya  Maendeleo  Ya Jamii Jinsia Wazee  na Watoto  Dk. Faustine  Ndugulile  (pichani), amesema, Serikali ina mpango wa kuanza kutoa oparesheni za ubongo nchini kwa kutumia matundu ya ubongo ili kupunguza athari za kiharusi.

Ndugulile amesema hayo jijini  Dar es Salaam mara  baada ya kutembelea mabanda yaliyo chini  ya Wizara hiyo, katika maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF)  yanayoendelea katika barabara ya Kilwa. 

Amesema serikali inaiagiza Muhimbili  kufanya tafiti  kwa magonjwa  yanayosambazwa na mbu kwani amekuwa  akibadilika  sana kitabia. 

"Kuna mbu  anaitwa Aedes anayeeneza ugonjwa  wa Dengue, mwingine Anofeles akisambaza malaria n'a yule  wa matende n'a mabusha...waliokuwa wakiuma mchana  wamebadilika n'a kuuma usiku  n'a vivyo  vivyo  kwa wale  waliokuwa wakiuma usiku, " Amesema Ndugulile.

Amesema mabadiliko hayo  ya mbu  inatakiwa utafiti, kwani mbu waliokuwa  wakikaa  ndani sasa wapo nje, n'a wale  waliofikiriwa  kuuma ndani  tuu  kumbe  sasa  wanauma  nje. 

"Nafikiri kuna mbu  wa ndani  tuliokuwa tukiwakinga kwa chandarua  lakini ikabainika  kwa sasa  wanauma nje hivyo jitihada za  kuhamasisha matumizi  y'a chandarua ikawa hayana tija,  mbu wengine  waliokuwa wakiruka juujuu sasa wanaruka chinichini, "amesema.

Amesema watafiti hao wafanye  utafiti kuangalia tabia hizo pamoja na dawa  zinazoweza kuua  mbu pamoja na viuadudu kama vinafanya  kazi  nzuri. 

"Katika banda  la Muhimbili wanaonyesha dawa za  kufukuza  mbu  n'a hata  mafuta ya kukupata kwa  ajili  ya kufukuza mbu," amesema. 

Amesema Hata Taasisi  y'a Utafiti  wa Magonjwa  yanayosambazwa Binadamu  (NIMR)  tumeshawambia katika kutekeleza  suala  hilo. 

Kuhusu operesheni za  ubongo  alisema  Taaisi y'a Mifupa y'a MOI inafanya  operesheni  hizo  n'a wapo  wataalam  waliokwenda  Nchini  China  wakitarajiwa  kurudi hivi  karibuni. 

Amesema operesheni  hizo  itakuwa za tundu  Ndogo, wakiziba damu katika mishipa  n'a kupunguza  athari  za kiharusi.

No comments:

Post a Comment

Pages