July 11, 2019

Wafanyabiashara Kutumia Fursa kutoka NMB

 Meneja Mwandamizi Uhusiano Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Wogofya Mfalamagoha akizungumza wakati wa mkutano wa NMB na Wafanyabiashara (NMB Business Club) mjini Babati Mkoani wa Manyara.
 Mfanyabiashara Ophii Urasa akizungumza wakati wa mkutano wa NMB(NMB Business Club) na wafanyabiashara wanaonufaika na mikopo ya benki hiyo kwa wilaya za Babati, Hanang na Mbulu mkoani Manyara.


Na Mwandishi Wetu
 
Mbunge wa jimbo la Babati Mjini,Pauline Gekul amewataka wafanyabiashara kutumia fursa ya kuendeleza biashara zao baada ya serikali kuondoa mlolongo wa tozo mbalimbali zilizokua zikitozwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kabla ya kufungua biashara.

Akizungumza katika mkutano uliondaliwa na benki ya NMB kwa wafanyabiashara mkoani Manyara (NMB Business Club) mjini Babati alisema waache kulalamikia mazingira ya biashara kwani katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 serikali imesikiliza kilio chao.

Nawapongeza NMB kuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara na kuwapa maarifa ya mikopo na kukuza biashara zenu,naamini mtaendelea kutoa mikpo zaidi kwa wananchi wangu ili waweze kujiletea maendeleo kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi,”alisema Gekul
Meneja Mwandamizi wa NMB Wogofya Mfalamagoha alisema NMB ipo tayari kuwahudumia wafanyabiashara wa ngazi zote kutokana na mtandao uliosambaa nchini nzima ikiwa na matawi zaidi ya 228 na mawakala 6,800.

“NMB ina wafanyabiashara zaidi ya 200,000 nchi nzima ambao wamechukua mikopo yenye thamani ya Sh 600 bilioni,mtakubaliana name kuwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo tunaifanya kuwaelimisha mambo ya biashara imekua na tija kwetu sote,”alisema Mfalamagoha.

Aliwataka wafanyabiashara kutokutanguliza dhamana zao wanapotaka kuchukua mikopo bali wazo la biashara ambalo linaweza kuwaletea faida kwani benki haipendi kuuza dhamana za wateja baada ya kushindwa kurejesha mikopo waliyochukua.

Alisema shughuli za wafanyabiashara wadogo na kati ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi ikizingatiwa kuwa uchumi kwa ujumla wake unategemea mafanikio ya shughuli za kibiashara zinazofanywa na wafanyabiashara wadogo na kati nchini na duniani.

“Lengo la kukutana nanyi ni kuhakikisha mnakuza mitaji yenu, kutoa ajira kwa watanzania wengi zaidi na kuchangia uchumi kupitia ulipaji wa kodi na kwamba NMB imejipanga kuhakikisha inatoa huduma bora kwa jamii ya wafanyabiashara katika makundi yao,”alisema Mfalamagoha
Mwenyekiti wa wafanyabiashara(NMB Business Club) Mkoa wa Manyara, Ally Msuya alisema wamekua na mahusiano mazuri na NMB hiyo kupitia umoja wao ambao wameutumia kutatua changamoto za wafanyabiashara wanaochipukia na wenye uzoefu wa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Pages