July 11, 2019

POLISI SITA MKOANI TABORA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

NA TIGANYA VINCENT

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) inatarajia kuwafikisha mahakamani Askari 6 wa Jeshi la Polisi na watendaji watatu wa vijiji wilaya Igunga baada ya kuomba rushwa shilingi milioni 8.

Akizungumza na vyombo mballimbali vya habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani Tabora Musa Chaulo alisema kwamba watu hao watafikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi kumamilika.

Alisema kwamba watendaji hao wa serikali wasio waaminifu walimuomba rushwa mzee Ngaka Mataluma Fale (95) baada ya kumukamata wakimtuhumu kuwa anajihusisha na tiba asilia bila kibali, kukutwa na mfupa unaodaiwa kuwa binadamu, kumiliki silaha za moto , kukutwa na mafuta ya simba, ngozi ya kengee na kukutwa na bangi.

Chaulo alisema baada ya Fale kukosa kiasi hicho cha fedha alitakiwa kuuza ng’ombe ili apate kiasi hicho cha milioni 8 kwa ajili ya kutoa hongo kwa Maafisa waliomkamata.
Aliongeza kuwa TAKUKURU ilifanikiwa kuwakamata ng’ombe kumi na mmoja wa Fale katika Mnada wa Igunga kwa wanunuzi wakijiandaa kuwasafirisha kwenda Arusha na kuongeza kuwa baada ya kuwakamata imewarajesha kwa mhusika.

Katika hatua nyingine Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani Tabora Chaulo amesema katika robo iliyoishia Juni , 2019 imefuatilia na kukagua miradi arobaini ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 9.285.

Alisema kati ya miradi hiyo saba inayohusu sekta ya elimu, afya na ujenzi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.570  inafanyiwa uchunguzi mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages