July 11, 2019

SAIDIENI TABORA KUWA KITOVU CHA BIASHARA-RC TABORA

NA TIGANYA VINCENT

WADAU wa maendeleo Mkoa wa Tabora wametakiwa kuandaa mpango mkakati utakaougeuza mkoa huo kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji  ili kuchangia na kuinua uchumi wa Taifa kwa kuwaunganisha  wajasiriamali na wawekezaji wakubwa
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wa kujadili na kutengeneza mkakati wa kuboresha mazingira ya uwekezaji mkoani humo

Alisema mipango hiyo ni lazima ilenge kuongeza uzalishaji wa malighafi mbalimbali zikiwemo za kilimo ambazo zitasaidia ujenzi wa viwanda ili kuongeza thamani na tija kwa wakulima.

Mwanri alisema kwamba uchumi wa kati wa viwanda, utakuza maendeleo endelevu na kuuwezasha Mkoa kuwa  na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora ambazo zinaweza kuuzwa nje ya nchi.

Alisema ili Taifa  liweze kuufikia uchumi wa kati, ni lazima sekta binafsi ziimarishwe ili ziwe na uwezo wa  uzalishaji mali  kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo ambavyo ndiyo msingi wa ukuaji wa viwanda vikubwa na unaozalisha bidhaa zinazotumiwa nchini.

Naye Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Magharibi  (TIC) Innocent Kahwa alisema asilimia kubwa ya pato la watu binafsi linategemea  wawekezaji  na wafanyabiashara  wadogo na wakati .

Alisema ili kupata mafanikio katika uwekezaji ni vema kujenga mazingira ya kuaminiana kati ya sekta binafsi na Serikali ili kila pande ifanye kazi zake kwa uhuru na kuwawezesha wajasiriamali kupata ubia.

No comments:

Post a Comment

Pages