HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2019

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi, akizungumza na Wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu  kwa alama vidole.
 Wananchi wakipata huduma katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi, akitoa huduma kwa mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.


Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi  ya TCRA Mabel Masasi  amesema ni fursa kwa wananchi wa Bukoba kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Masasi amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Masasi.

No comments:

Post a Comment

Pages