Sehemu ya watalii kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka, wakiwa katika picha tofauti kwenye kilele cha milima ya Matogolo.
Sehemu ya watalii kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka, wakiwa katika kilele cha milima ya Matogolo.
Sehemu ya watalii kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka, wakiwa kwenye kilele cha milima ya Matogolo.
Kwenye picha tofauti watalii kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka, wakiwa katika chanzo cha Mto Ruvuma, kinachopatika kwenye misitu minene ya milima Matogolo, Songea.
Kwenye picha tofauti watalii kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka, wakiwa katika chanzo cha Mto Ruvuma, kinachopatika kwenye misitu minene ya milima Matogolo, Songea.
Na Mwandishi Wetu, Songea

INGAWAJE serikali ya Mkoa wa Ruvuma imetoa fursa kwa wananchi
wake kutembelea vivutio vilivyomo mkoani humo, bado mwamko wa wananchi ni
hafifu, huku Tamasha la Majimaji Selebuka likipewa heko na Mkuu wa Wilaya wa
Songea, Poreleti Kamando kwani limekuja kubadili ‘upepo’.
Takwimu zinaonesha kwa mwaka wastani wa kupokea watalii ni
mara kumi tu, licha ya mkoa wa Ruvuma kujaaliwa utitiri wa vivutio vya kitalii asilia,
kama vile Misitu minene ya Matogoro, chanzo cha mto Ruvuma kilichopo mpangilio
ya milima ya Matogoro, mabawa ya samaki, makumbusho ya Waziri Mkuu wa Kwanza wa
Tanzania, Hayati Rashid Kawawa, Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji
1905 na vingine vingi.
DC Kamando amepongeza Taasisi ya So-Mi ambayo huratibu
Tamasha la Majimaji Selebuka kila mwaka ambalo mbali na shughuli nyingine,
sekta ya utalii imepewa kipaumbele zaidi kama njia ya kuhamasisha utalii wa
ndani.
“Katika kutangaza utalii, tamasha hili limekuwa likiisaidia
serikali kutekeleza ilani ya serikali ya sasa, ili kupitia vyombo vya habari
Tanzania nzima iweze kujua vivutio vilivyopo Ruvuma na kusini mwa Tanzania kwa
ujumla.
“Tunaamini kupitia tamasha hili, watu watavutika na
watatembele vivutio vyetu na hawahawa watakuwa mabalozi huko waendako.
“Kwa niamba ya serikali, nawashukuru kwani mnatutendea mema
na kutekeleza yale yaliyo kwenye mipango ya serikali yetu na hii inatupa nafasi
ya kutangaza fursa ya utalii tulionayo Ruvuma,” alisema Kamando.
Kwa mwaka huu, ziara ya utalii wa ndani ilikuwa kwenye misitu
minene ya milima ya Matogoro pamoja na kwenye chanzo kikuu cha Mto Ruvuma
kilichopo nyanda za juu kwenye milima ya mpangilio ya Matogoro.
Kwa
mujibu wa Lekoko Olenjilalo, Mhifadhi Misitu Msaidizi Mkoa wa Ruvuma,
alisema wastani wa kupokea watalii kwa mwaka ni mara kumi.
“Ukweli mwamko ni mdogo, pamoja na kwamba hakuna kiingilio
lakini bado. Wastani kwa mwaka utakuwa tunapokea watalii mara kumi hadi kumi
tano na asilimia kubwa ni viongozi tu, kwa wananchi wa kawaida suala la utalii
kwao bado,” alisema Lekoko.
Profesa Julian Murchison, raia wa Marekani ni miongoni mwa
waliokwenda kutalii milima ya Matogoro: “Hii ni safari yangu ya kwanza kufika
hapa, ila nimefurahi sana kuona mazingira ya hivi (mwamba mweupe kileleni mwa
milima ya Matogoro). Mazingira yanavutia, kuna upepo mzuri kileleni na pia
kuona chanzo cha mto mkubwa (Ruvuma), inapendeza kwa kweli.”
No comments:
Post a Comment