Zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 zimekusanywa na
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa Mwaka Fedha 2018/2019 ambazo ni zaidi ya asilimia 97 za mapato kwa mwaka mzima.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bukoba, Murshid Hashim Ngeze (pichani), katika kikao
cha halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri uliopo mkoani
hapa kilicholenga kufunga robo ya nne ya
mwaka wa fedha 2018/2019.
Ngeze amesema kuwa Halmashahuri
hiyo imepiga hatua kubwa na kudai kuwa kuwa wakati wanaingia madarakani walikuwa
wakikusanya zaidi ya shilingi milioni
mia sita kwa mwaka lakini mpaka sasa wamevuka malengo kwa 100% kwa miaka minne
wakiwa kwenye uongozi.
‘’Ni jambo la kumshukuru mungu nikikumbuka tulipoanzia hadi sasa
ni hatua kubwa hii ni kutokana na juhudi kubwa za Rais wetu za mapambano yenye
kuleta maendeleo amesema’’
Amesema kuwa mafanikio hayo
yamekuja kutokana na kasi ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika ya kusimamia vizuri rasilimali mbalimbali za nchi na ndio sababu kila kiongozi amewajibika kwa nafasi yake
kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote
ujumla.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Rukoma amesema
kuwa tayari ujenzi wa shule ya sekondari
umeanza katani Rukoma ili kutatua
changamoto inayowakabili wanafunzi wa kata hiyo wanaangaika kufata huduma ya
elimu umbari mrefu unaowalazimu kutembea takribani kilometa 38.
Hata hivyo Ngeze ametoa wito kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii
ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa zima kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment