Picha tofauti zikiwaonyesha
waandamanaji walioandamana katika Ubalozi wa Afrika Kusini kushinikiza
kuachiwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) inayoshikiliwa Jijiji Johannesburg
nchini
Afrika ya Kusini.
Waandamanaji.
Mmoja wa waandamaji akiwa na bango lake.
Askari Polisi wakiwatuliza waandamanaji katika Ubalozi wa Afrika
ya Kusini hapa nchini waliokuwa wakishinikiza kuachiwa kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) inayoshikiliwa jijini Johannesburg
Afrika Kusini. (Na Mpiga Picha Maalum).
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Katika hali isiyo ya kawaida
mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameandamana kuelekea katika Ubalozi
wa Afrika ya Kusini nchini kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya ATCL
inayoshikiliwa Jijini Johanesberg Afrika ya Kusini kwa amri ya Mahakama.
Maandamano hayo ambayo hayakufahamika yametokea upande gani wa Jiji
yaliwashirikisha watu mbalimbali wakiwemo waliojitambulisha kama wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya Juu pamoja na wananchi wa kawaida waliodai wamechoshwa na vitendo vya kuihujumu
serikali ya awamu ya Tano.
Mabango mbalimbali waliyobeba
waaandamanaji hao yalionyesha kusikitishwa na kitendo cha kushikiliwa kwa ndege
ya Tanzania nchini Afrika ya Kusini , nchi ambayo uhuru wake umepatikana kwa
msaaada wa Tanzania kwa kuwasaidia makazi na hata vifaa waliokua wapigania
uhuru wa nchi hiyo.
Mmoja wa waandamanaji hao ambaye
hakutaka kutaja majina yake , akiongea kwa uchungu alisema Afrika ya Kusini imekua
nchi isiyo na shukrani kabisa kwa kitendo cha kuikamata ndege ya ATCL ambalo
ndilo kwanza linatoka katika hali ya kuwa taabani.
“Tumekuja hapa kuwaambia wenzetu
wa Afrika ya Kusini kwamba uungwana sio tu kulipa fadhila kwa aliyekusaidia,
bali hata matendo tu yanatosha, haiwezekani sisi tumewasaidia wapate uhuru leo
hii hawana hata aibu wanakamata ndege yetu tena kwa sababu zisizokua na msingi”
Alisema mmoja wa waandamanaji hao.
Mingoni mwa mabango waliyobeba
yalisomeka ‘Turudishieni ndege yetu na sisi tuwarudishie makaburu uhuru wao
maana mmeshindwa kuwa wasataarabu’ lingine lilisomeka ‘ Waafrika ndio maana
tunadharaulika duniani kwa kufanya mambo ya hovyo.
Kwa upande wake Sadik Ramadhan
aliyekua anazungumza kwa jazba alisema waafrika ya kusini ni rafiki zetu
kitendo cha kushirikiana na mzungu mmoja kuihujumu Tanzania ni kitendo
ambacho hakikubaliki kabisa, alisema
Rais Ramaphosa alipokuwa nchini kwenye mkutano wa SADC aliwahakikishia
watanzania kwamba undugu wa nchi hizi utaendelea na hakuna hata mtu mmoja wa
kuuvunja.
Aidha alisema lengo la maandamano
hayo ya amani ni kumtaka Balozi atoke na aeleze ni hatua gani zinazoendelea za
kuhakikisha ndege ya watanzania inarudi kwani imenunuliwa kwa kodi za wananchi
tena wananchi masikini wanaopambana kuinua nchi yao.
Huku wakiimba wimbo kwamba
wamemsaliti mzee Mandela waandamanaji hao walisema inatia uchungu sana kuona
taifa lililosaidiwa na Tanzania ndio sasa linakua mstari wa mbele kuhujumu mali
zake jambo ambalo wamesema halikubaliki.
Maandamano hayo ambayo yalizua
taharuki kwa takriban nusu saa, yalizimwa na Jeshi la polisi kwa kuwataka
waandamanaji hao kuondoka kwa madai suala hilo linaendelea kushughulikiwa kwa
mujibu wa sharia na taratibu za kidiplomasia.
Baada ya kuamriwa kuondoka
waandamanaji walitawanyika wakiendelea kuimba kwamba ujume umefika na
kilichobaki wanasubiria ndege yao na kama haitaachiwa watafanya ubalozi huo
ushindwe kutekeleza kazi zake za kila siku kwani wataandamana mpaka kieleweke.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa alipofika kwenye ubalozi huo
aliwataka waandamanaji kufuata sharia na kutojichukulia sharia mkononi kwani
wanaweza kushitakiwa, aidha Jeshi la Polisi liliwatia nguvuni baadhi ya
waandamanaji hao.
Hadi maandamano hayo yanavunjwa
hakuna kiongozi yeyote wa ubalozi huo aliyejitokeza kusikiliza hoja za
waandamanaji bali walijifungia ndani huku baadhi ya wafanyakazi wakionekana
kuchungulia madirishani kuona nini kinaendelea , na wengine wakipiga picha kwa
kutumia simu zao za kiganjani.
No comments:
Post a Comment