Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwahutubia Madiwani wakati wa kikao
Maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/18.
NA TIGANYA VINCENT
MENEJIMENTI ya Halmashauri
ya Wilaya ya Tabora(Uyui) imepewa Mwezi
mmjoa kuhakikisha imejibu na kumaliza kujibu hoja 72 za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) zilizosalia ili ziweze kufungwa na
kuondoa dosari zilizojitokeza kwenye ukaguzi uliopita.
Hoja hizo zinahusu miradi
na manunuzi mbalimbali iliyotumia zaidi ya shilingi milioni 515.4 ambayo hayana
uthibitisho.
Agizo hilo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya
mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/18.
Alisema hoja hizo ndio
zimesababisha Halmashauri hiyo kuwa kati ya Halmashauri saba nchini zilizopata
Hati yenye shaka ni lazima zijibiwe kwa kuwasilisha vielelezo
vitakavyothibitisha matumizi ya fedha hizo kama yalifuata taratibu.
Awali akiwasilisha
taarifa Mkaguzi Mkuu wa Nje Anicet Mushumbusi alizitaja sababu zilizopelekea
kupata Hati yenye shaka kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uthibitisho wa fedha
za Amana kiasi cha milioni 30.4, malipo yenye shaka kwa kazi hewa ya shilingi
milioni 95.2.
Sababu nyingine ni
manunuzi ya shajala kwa ajili ya vikao mbalimbali yenye thamani ya shilingi
milioni 116.5 ambayo hayana mchanganuo na malipo yenye nyaraka pungufu kiasi
cha milioni 20.4.
Mushumbusi aliongeza kuwa
sababu nyingine ni pamoja na mapungufu kwa vidadisi bei zilizowasalishwa na
watoa huduma kabla ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya milioni
200.5 na manunuzi yaliyofanyika bila ushindanishashi ya milioni 52.2.
Naye Katibu Tawala Mkoa
wa Tabora Msalika Makungu alisema watawachukulia hatua watumishi wote ambao
wameisababishia Halmashauri hiyo kuzalisha hoja za kiukaguzi za kiukaguzi na
kupata Hati yenye shaka.
Alisema watumishi ni vema
wakajitahidi kuzuia hoja na zio kutoa maamuzi ambayo yanasababisha kuendelea
kuzalisha hoja kila mwaka.
Katibu Tawala Mkoa wa
Tabora aliitaka Menejimenti ya Halmashauri hiyo kuunda timu ya kushughulikia
hoja hizo ili ndani ya Mwezi mmoja wawe wamejibu na kufutwa.
Makungu aliwaomba Madiwani
kuhakikisha wanafuatia katika Kata zao ili miradi mbalimbali ya wananchi
inakuwa na ubora unaotakiwa.
Kwa upande wa Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) Said Ntahondi alisema wameunda timu
ya Madiwani na Wataalamu watakaochunguza watendaji waliosababisha wapate Hati
yenye shaka ili waweze kuchukuliwa hatua.
Alisema kuwa timu hiyo
inatarajia kukabidhi taarifa hiyo tarehe 22 Mwezi huu kwa ajili ya hatua
nyingine.
Ntahondi alisema lengo ni
kutaka kuondoa dosari zilizowasababisha wapate hati hiyo na kufanya vizuri
kipindi kijacho.
No comments:
Post a Comment