NA MWANDISHI WETU, DODOMA
TIMU
ya Dodoma Jiji FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL), leo
inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City, kwenye Uwanja
wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mchezo huo awali ulipangwa kupigwa Agosti 8 mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na mwingiliano wa ratiba.
Dodoma
Jiji FC ambayo msimu huu imefanya usajili wa kibabe kwa nyota kutoka
kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), wakiwa na lengo la kuipandisha
daraja msimu ujao.
Akizungumza
jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Dodoma FC, Fortnatus John alisema mchezo
huo utakuwa mahususi kwa ajili ya kujiweka fiti na msimu mpya wa Ligi
Daraja la kwanza utakaoanza Septemba 14.
Mechi
hiyo itapigwa saa 10:00 jioni, Wakati kiingilio kitakua Sh. 2,000 na
utakua mchezo wa kwanza wa Kocha Mbwana Makata kuiongoza timu hiyo tangu
alipokabidhiwa kuchukua mikoba ya Kocha Jamhuri Kihwelo.
"Huu
ni mchezo muhimu wa kujipima nguvu kama sehemu ya maandalizi ya Ligi
Daraja la Kwanza ambayo sisi tutashiriki na tumenga kuhakikisha
tunapanda Ligi Kuu.
"
Tumeweka kiingilio cha chini ili kila Mwana-Dodoma na mpenda soka aweze
kuja kuitazama Tltimu yake na kutoa hamasa kwa wachezaji wetu,
tunawaomba wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi ili kuiunga
mkono Timu yao ambayo sisi viongozi tunawahakikishia kuwa imesukwa
upya," amesema Fortnatus.
Alisema
mchezo huo pia utakua mahususi kwa ajili ya kutambulisha wachezaji
wapya wa kikosi hicho pamoja na benchi la ufundi kwa mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment