HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 04, 2019

SHULE ZA ATLAS ZASISITIZA MAADILI KWA WATOTO


Meneja wa Kudhibiti Viwango katika Shule za Atlas, Wilbroad Prosper, akizungumza katika kikao cha wazazi na walimu wa Shule ya Msingi Atlas iliyopo Madale jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wazazi wakiwa katika kikao hicho.

Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Atlas Madale.




Na Mwandishi Wetu

Shule za Atlas zilizopo Jijini Dar es Salaam zimewataka wazazi kuzingatia maadili miongoni mwa watoto hasa kipindi hiki cha likizo ya robo tatu ya mwaka.

Akizungumza katika kikao cha wazazi na walimu wa Shule ya Msingi Atlas Madale iliyopo Wilaya ya Kinondoni, Mkuu wa Shule hiyo, Sarah Nalubega, amesema kuwa watoto wengi wamekuwa na nidhamu mbaya jambo ambalo si jema kwa ustawi wa kifamilia na Taifa kwa ujumla.

"Unaweza kupishana na mtoto asikusalimie hii ni nidhamu mbaya sana, sasa unajiuliza hivi ndivyo wanavyofundishwa?" alihoji Mwalimu Nalubega.

Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi anayeshughulikia taaluma, Joseph Mjingo, alisema kuwa ushirikiano baina ya walimu na wazazi ni suala muhimu sana katika maendeleo ya mtoto kitaaluma.

Amesema kuwa pamoja na kuwepo maendeleo ya kiteknolojia na kiuchumi bado wazazi wanalo jukumu la kulea watoto kwa tamaduni za kiafrika kwa ustawi bora kabisa.

Alitolea mfano wa vipindi mbalimbali vya runinga kama vile katuni na kusema wazazi wanalo jukumu la kutoa mwongozo sahihi juu ya vipindi husika.

"Vipo vipindi vinavyojenga na vinavyopotosha ni jukumu letu wazazi kuwaelekeza watoto njia iliyo sahihi" alisema Joseph.

Mwalimu huyo wa taaluma alisema katika shule za Atlas ambazo zipo kampasi mbili ya Ubungo na Madale, mbali ya wanafunzi kufundishwa kusoma na kuandika vilevile hufundishwa ujuzi na stadi mbalimbali ili kuwasaidia wamalizapo masomo yao.

Ameyataja mambo muhimu mzazi anatakiwa kuzingatia kwa mtoto wake kuwa ni pamoja na mwandiko wake, kama anakusanya kazi zake ili kusahihishwa na ratiba ya shule

Naye Wilbroad Prosper ambaye ni Meneja anayeshughulikia viwango katika shule za Atlas amesema kuwa mbali ya maendeleo ya taaluma vile vile ipo haja ya kuangalia vipaji vya watoto.

No comments:

Post a Comment

Pages