Wazazi na walezi wa wahitimu wa
wanafunzi wa darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Msingi Jamia English
Medium Nursery And primary school
iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera
wametakiwa kumaliza deni la Sh. Milioni Saba wanalodaiwa kutokana na
ununuzi wa gari la shule kabla ya kupelekwa mahakamani.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 4, 2019 na mwenyekiti wa bodi ya
shule ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta katika
mahafali ya shule ya msingi Jamia
English Medium Nursery And
primary school wakati akielezea maendeleo ya shule hiyo.
Sheikh Kichwabuta amesema baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo
wamekuwa wakipigiwa simu mara kwa mara na wengine kuandikiwa barua
zinazowahimiza kukamilisha deni hilo ambapo wazazi hao wamekuwa wakahidi.
Akielezea Deni linaloikabili shule
hiyo amesema lengo na madhumuni ya kuletwa kwa gari hilo shuleni hapo ilikuwa
ni kuwasaidia watoto wanaoenda shule na kurudi nyumbani baada ya masomo
kutokana na wanafuzi hao kupata adha kubwa ikiwemo jua kali umbali mrefu na
Mvua.
Amesema kuwa jambo la kushangaza gari
hilo licha ya kuwepo shuleni hapo wazazi hawalitumii ambapo wanadai kuwa watoto
wao watatembela miguu ambapo wengine utoka mbali na kusababisha kuchelewa
kufika shuleni hapo.
Kutokana na deni hilo mwenyekiti huyo
amesema kuwa uwezekano wa kuwafikisha wazazi hao mahakamani ni mkubwa sana huku
akiwataka baadhi ya wazazi wengine kumalizia ada za watoto wao wanaohitimu
Elimu ya msingi ili kusaidia wanafunzi wanabakia shuleni hapo kusoma kwa amani.
‘’Mimi
siwezi kupigwa presha bure Hawa wanafunzi wanamaliza mwaka mzima mtoto analipa laki moja zimeandikwa barua ya
kuwataka mara kwa mara kulipa michango hiyo lakini wazazi hamkutii tuwapeleka
mahakamani wazazi walioshindwa kulipa michango ya shule ikiwemo deni la gari la
shule’’amesema.
kwa upande wao baadhi ya wazazi wa wahitimu
hao ambao hwakupenda majina yao yatajwe wameiomba shule hiyo kuwasamehe ili
waanze kulipa kidogo kidogo.
kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule
hiyo Bi Nuriat Nuru amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma
licha ya changamoto mbali mbali ikiwemo ulipaji mbaya wa ada ya shule kwa wazazi,
chumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike.
Wahitimu hao wametoa pongezi kwa
uongozi wa shule hiyo kwa kuwapatia elimu nzuri yenye maadili na kuwaomba
wazazi wao kuona umuhimu wa kuchangia maendeleo ya shule.
Wametoa pongezi kwa mwalimu wa taaluma
na mfundishaji wa somo la kiingereza
Shakiru Kalembalemba kwa kuwatoa mbali na kuwaivisha katika lugha
hiyo.
Akijibu suala hilo la deni la shilingi
milioni 7 la gari hilo mgeni rasmi katika mahafali hayo Mhandisi Nasir Chakindo
amechangia shilingi laki 3 na kuungwa mkono na wadau mbali mbali waliochangia
shilingi laki 7 huku akiwataka wazazi hao kuchangia maendeleo ya shule ili
kutowavunja moyo walimu.
No comments:
Post a Comment