Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Wataalamu wa Sekta ya Manunuzi ya Umma nchini wametakiwa kwenda na
mfumo mpya wa manunuzi ili kuendana na mnyororo wa thamani ya fedha
wenye uwazi utakaosaidi serikali kutekeleza bajeti kwa kuokoa na
kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro wakati
akifungua mafunzo ya wataalamu wa sekta ya manunuzi juu ya mfumo mpya wa
manunuzi ya umma kwa njia ya mtandao na kuzitaka taasisi za serikali
kuchangamkia fursa ya kuleta wataalamu wao kupata mafunzo
hayo.
Alisema kuwa mfumo huo utasaidia sana kuondoa misururu maofisini na
kuipunguzia serikali gharama na hivyo mnyororo wa thamani ya fedha
kuonekana na kuwapunguzia kutopatikana kwa nwazabuni wasioendana na
miradi pia wao kuwapunguzia majukumu ya ufuatiliaji wazabuni hao
wanaotekeleza miradi na huduma chini ya viwango kila uchwao.
“Najua wapo wengine watachukia ila kuweni na uzalendo kwa kuwa mfumo huu
utawasaidia kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa upande wenu na
utajenga usawa wa kuwapata wazabuni wenye ubora na sifa sahihi hali
itakayopelekea kuokoa fedha za serikali”
Alitanabaisha kuwa mfumo huo ni kama moyo wa serikali hivyo mafunzo
mtakayoyapata ni matarajio yangu yataenda kuleta mafanikio chanya
nikiamini kuwa wapiga dili hawataupenda mfumo huu kwa kuwa matumizi
mabaya ya serikali yanaanzia huko kwenye manunuzi ya umma.
Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya Mtendaji mkuu wa mamlaka ya usimamizi
wa manunuzi ya umma PPRA mhandisi Leonard Kapongo alisema kuwa mafunzo
hayo ni ya awamu ya nne tokea kuzinduliwa kwa mfumo huo ambao upo
kisheria na utasaidia kuongeza uwelewa ili kutekeleza jukumu la takwa la
kisheria.
Alisema kuwa jumla ya washiriki 220 kutoka taasisi 71 wanapatiwa mafunzo
hayo kwa siku sita awali mafunzo hayo yalianza kwa taasisi 80 kutoka
mikoa mitano tokea mwezi wa nane mwaka huu na kusema kuwa hii ni awamu
ya nne tokea mafunzo hayo kuanza na yanatolewa bure.
No comments:
Post a Comment