HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 21, 2019

CRDB yatumia AALCO kujitangaza


Na Suleiman Msuya

BENKI ya CRDB ambayo ni mdhamini wa Mkutano Mkuu wa 58 wa mwaka wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria ya nchi za Afrika na Asia (AALCO) imesema itautumia mkutano huo kujitanga na kutanua soko la biashara.
Hayo yamesemwa na Meneja Mwandamizi Idara ya Serikali za Mitaa CRDB, Suzan Shuma, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo mkutano huo unafanyika.
Shuma alisema benki hiyo inatembea na kauli mbiu yao ya ulipo tupo hivyo inaamini ushiriki wake katika mkutano huo wataweza kujitangaza kwa nchi shiriki.
Alisema kwa sasa CRDB inapatikana Tanzania na nchini Burundi hivyo ni wazi kuwa siku chache zijazo wataweza kufikia nchi nyingine.
“Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa maendeleo ambapo inashiriki miradi mingi ya Serikali hivyo kupitia mkutano huu wa AALCO tunatarajia kujitangaza zaidi kibiashara,” alisema.
Shuma alisema katika mkutano huo wa AALCO benki hiyo itakuwa inatoa huduma ya kutoa na kubadilisha fedha na kutoa kadi.
Alisema mikakati ya benki hiyo ni kuendelea kuwa kinara wa kutoa huduma za kibenki nchini na nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome alisema CCDB ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.
Alisema Serikali inaipongeza benki hiyo kujitokeza kudhamini mkutano huo na kwamba haijakosea kufanya hivyo kwa kuwa mkutano huo ni fursa ya kujitangaza kimataifa.
Mkutano wa AALCO unashirikisha nchi 49 za Bara la Asia na Afrika ambapo viongozi katika Sekta ya Sheria hukutana na kujadiliana namna ya kutatua changamoto za kisheria na haki za kibinadamu kwenye nchi wanachama.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO), jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO), jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO) uliofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.

Washiriki wa mkutano.

Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

Washiriki.
Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa pili kulia) akifuatilia mkutano huo pamoja na wafanyakazi wenzake.



Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akizungumza katika mkutano huo.



Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano huo Benki ya CRDB.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya CRDB.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB, Suzan Shuma.

Meneja Mwandamizi Benki ya CRDB, anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa, Suzan Shuma, akizungumza na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Pages