MBUNGE wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea amesema anatarajia kumwandika barua Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kutokana na kuzuiliwa kufanya shughuli zake za kijimbo katika Jimbo lake.
Miongoni mwa shughuli zake alizozitaka kuzifanya hivi karibuni ni pamoja na kuwaelezea wananchi changamoto iliyokwamisha ujenzi wa Daraja la mto Gide lililopo katikati ya Makoka na Kimara Baruti ambapo mvua zilizonyesha juzi zilileta maafa na mtoto ajulikanae Rashid Makoye alitumbukia katika daraja hilo na mwili wake kushindwa kuonekana hadi leo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa ugawaji wa mihuli ya Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA )katika jimbo lake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Kubenea anasema atamwandikia barua msajili huyo na kumuambatanishia barua zote za polisi na video za juzi alizozuiliwa asifike katika Mkutano wake na wananchi.
Pia anasema anapeleka barua kwa Spika wa Bunge rasmi Job Ndugai ili awasilishe malalamiko yake kwa Rais,John Magufuli .
“Kama madai haya hayatasikilizwa nitakishawishi Chama changu cha CHADEMA kiandike malalamiko rasmi kwenye Jumuiya ya Kimataifa," alisema na kuongeza
“Ni kweli tumechoka kuzuiliwa huku kwa mikutano haya tunayofanyiwa yamepitiliza na kudhoofishwa juu zangu za kuwaletea maendeleo wananchi katika jimbo langu…… licha ya yote ninayopitia nawaambia kuwa Ubungo nimejipanga nakuhakikisha tutapata wagombea wa nafasi zote na tutashida ,”anasema Kubenea
Aidha anasema anaamini kuwa anazuiliwa kufanya mikutano katika jimbo lake kwa sababu yeye ni miongoni mwa wabunge wanaofanya kazi kubwa ndani ya kipindi kifupi ya kuwatumikia wananchi na kuwapelekea maendeleao.
“Nimetumia fedha ya mfuko wa jimbo kuwapatia maendeleo wananchi wa jimbo langu kwa kuwawezesha baadhi ya vikundi vya vijana na wakinamama kuwapatia fedha za kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo,’’anasema na kuongeza
“Mfuko ulitoa Milioni nane kwa ajili ya kujenga kisima katika Shule ya msingi Mabibo na kutoa Milioni 12 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima katika soko la Gamesi lilipo Mabibo ili wafanyabiashara wa soko hilo wapate maji,”anasema
Wakati huo huo Kubenea aligawa mihuri 46 ya mitaa yote ya jimbo lake ambayo itatumika katika ujenzi wa Chama na kwenye Uchaguzi wa Serikali ya mitaa ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni.
“Nagawa mihuri hii kwa jimbo zima na hii mihuri inafanana yote na ugawaji huu ni dharula kutokana na moja ya vipengele vilivyopo katika uchaguzi wa mwaka huu wa serikali ya mitaa ya kutaka mgombea kuwa na muhuri wa mdhamini wa ngazi ya chini ya Chama ambayo ni Tawi,”anasema Kubenea
No comments:
Post a Comment