HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2019

Watumiaji barabara Shekilango, Bamaga wafundwa


Mratibu wa Ujenzi wa Barabara ya Shekilango kutoka Kampuni ya CRBC , Yung Steven, akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikati), barabara ya mchepuko iliyoanza kufanyiwa matengenezo katika eneo la Sinza Makaburini jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Uenezi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani (SP), Abel Swai.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kampuni CRBC, Yung Steven, muda mfupi kabla hajafungua mafunzo ya utoaji elimu kwa watumiaji wa Barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kampuni CRBC, Yung Steven, muda mfupi kabla hajafungua mafunzo ya utoaji elimu kwa watumiaji wa Barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Uenezi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani (SP), Abel Swai, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji elimu kwa watumiaji wa Barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa barabara ya mchepuko Sinza Makaburini ambayo imeanza kukarabatiwa na Kampuni ya CRBC .

Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria mafuzo ya elimu ya usalama barabarani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo.

Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria mafuzo ya elimu ya usalama barabarani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya utoaji elimu kwa watumiaji wa Barabara ya Shekilango ambayo ujenzi wake utakuwa wa barabara nne.




Na Mwandishi Wetu


WANANCHI wanaoishi na kutumia barabara ya Shekilango Kata ya Sinza wilayani Ubungo wametakiwa kuwa walinzi wa malighafi zitakazotumika kwenye ujenzi barabara hiyo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Daniel Chongolo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wanafunzi wa shule za Makumbusho, Mugabe, Loqman, Reginald Mengi, waendesha bodaboda na bajaji.

Alisema mafunzo hayo yaliondaliwa na Kampuni ya ujenzi ya China Road and Bridge Corporation (CRBC) kwa kushirikiana na Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam (DMDP) yana lengo kuwajengea uelewa watumiaji wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 3.7 kutambua umuhimu wa kulinda vifaa na matumizi sahihi kipindi cha ujenzi.

Alisema ili mradi huo uwe na matokeo chanya ni lazima wananchi kuwa walinzi wa vitendea kazi ambavyo vitatumika katika ujenzi na sio kuviiba.

"Serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu wa Shekilango hadi Bamaga ambao umegharimu zaidi ya Sh.Bil.32, ombi langu kwenu ni kuhakikisha mnakuwa walinzi wa vitendea kazi ili kazi imalizike kwa wakati," alisema.

Aliwapongeza CRBC na DMDP kuamua kutoa elimu kabla ya ujenzi kuanza na kuwataja wajenzi wengine kuiga mfano huo.

 
Chongolo aliwataka washiriki wa elimu hiyo kuchukua kwa uzito mafunzo hayo ili wakawe mabalozi wazuri kwa siku zijazo.

Alisema matumizi salama ya barabara ni vema yakazingatiwa wakati wa mradi ili kuepuka ajali huku akiwaelekeza waendesha bodaboda na bajaji kuacha ujuaji wa kila jambo bali wafuate sheria za barabarani.

Chongolo alisema takwimu za mwaka jana zinaonesha Wilaya ya Ilala imepata ajali za bodaboda 223, Kinondoni 212 na Temeke 163 zikiwa ni ajali nyingi kuliko ajali zilizopatikana kwenye mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Shinyanga jambo ambalo linasikitisha.

"Acheni matumizi mabaya ya barabara kwani ajali zinawaletea ulemavu na kuwa tegemezi nyie na familia zenu," alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Uenezi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani SP Abel Swai, alisema wamejipanga kushirikiana na wajenzi ili kuepusha foleni.
 
Swai alisema iwapo watumiaji barabara watapata elimu ni dhahiri watakuwa walinzi wa mradi huo ambao utapunguza foleni.

"Ni vema madereva watumie alama za barabarani ipasavyo na sio kulazimisha makosa ambayo sio ya lazima," alisema.


Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Kampuni CRBC, Yung Steven alisema wameamua kutoa elimu kwa wananchi ili kurahisisha ujenzi.


Alisema iwapo mvua hazitaendelea mradi utakamilika kwa wakati huku akiwataka wananchi wanaoishi maeneo jirani watoe ushirikiano.


"Mradi huu tumepewa na DMDP tunatarajia kuumaliza haraka ndio maana tumeona tuwape elimu wananchi kabla ya kuunza," alisema.


Aliisema ujenzi huo utahusisha barabara za michepuko za Makaburini, Mori, Akachube na TRA ambazo ujenzi umeshaanza tangu mwezi Juni mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages