JESHI la Polisi limewahakikishia wananchi uwepo wa usalama kipindi chote cha mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa kuanzia kwenye zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura, upigaji kura na utangazaji wa matokeo.
Aidha limewataka askari kuzingatia maadili yao ya kazi wakati wanalinda amani huku likiweka wazi kuwa hawatakuwa wakipendelea upande wowote wakati wa mchakato huo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, (RPC), Jonathan Shanna, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake juzi akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dk. Maulid Madeni, ambapo alisema hali ya usalama ilikuwa shwari katika kipindi chote cha uandikishaji.
Alisema kuwa idadi kubwa ya askari polisi wamejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.
"Jeshi la polisi mkoani Arusha hatutakuwa na upendeleo kwa chama chochote cha siasa, kwa mtu yeyote, kwa dini yoyote, kwa kabila au jinsia yoyote," alisema kamanda Shanna.
Aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha baada ya muda wa zoezi hilo la uandikishaji kuongezwa ambapo zoezi hilo litahitimishwa oktoba 17, mwaka huu badala ya oktoba 14, mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Kamanda Shanna alisema pamoja na tarehe za kujiandikisha kusogezwa mbele na waziri mwenye dhamana ya uchaguzi huo Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Selemani Jaffo lakini siku ya kupiga kura ni ile ile ya awali.
"Wananchi watumie fursa hii kujiandikisha ili waje watumie haki yao ya kikatiba kupiga kura kuchagua kiongozi wanayemtaka," alisema kamanda Shanna akijibu maswali ya waandishi wa habari na kuongeza.
" Mimi mwenyewe nimejiandikisha nitapiga kura kwa sababu ji haki yangu na askari wangu wengi wamejiandikisha pamoja na familia zao lakini siwezi kuwaeleza wapigie kura chama au mtu gani huo ni uhuru wao wala sipaswi kujua,".
Oktoba 13, mwaka huu Waziri Jaffo akijiandikisha kupiga kura kwenye kitonhoji cha Kimani wilayani Kisarawe mkoani Peani aliongeza siku za uandikishaji mpaka oktoba 27, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment