Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi
(katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi
karibuni. Kulia ni Dk. Hamza Kabeho Mkurugenzi wa Utabiri.
Na Irene Mark, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa siku mbili.
Angalizo hilo limetolewa leo Oktoba 16 na kutaja maeneo yatakayokumbwa na mvua hiyo kuwa ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa kutoka TMA zimesema mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi Oktoba 17,2019 hivyo wakazi wa mikoa tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Kwa sababu hiyo athari zitakazotokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

No comments:
Post a Comment