Mwendesha Bodaboda, Masoud Seif, akiwa ampempakia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati wa uzinduzi wa huduma ya NMB Masta Boda iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna na kushoto ni Mrakibu wa Polisi (SP), Abel Swai. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ameipongeza Benki ya NMB kwa ubunifu wa huduma mpya, ya kisasa, nafuu na salama ya malipo ya kielektroniki ijulikanayo kama NMB MastaBODA.
Waziri Mhagama alitoa pongezi hizo wakati azinduzi wa huduma hiyo, inayotolewa na NMB kwa kushirikiana na Mastecard QR, ambako aliwataka, madereva bodaboda wote nchini, kuchangamkia huduma hiyo inayolenga kuirasmisha sekta ya usafirishaji kwa njia ya pikipiki.
Alibainisha, jamii imekuwa ikiutazama usafiri wa bodaboda kama usio na hadhi, huku wakiwachukulia watoa huduma hiyo kuwa ni watu wasio waadilifu lakini kupitia NMB MastaBODA, unaenda kuupa hadhi usafiri huo.
“Nguvu kazi ya taifa ya vijana nchini asilimia 56, wengi wao wanahudumu katika sekta ya usafiri wa bodaboda, alisema na kuongeza kuwa ...Huduma hii inaenda kulirasimisha kundi hilo na inaisaidia Serikali katika kutanua milango ya ajira kwa vijana nchini kwa kumiliki pikipiki za mikopo, kujiajiri wenyewe na wao kuajiri wengine.”.
Waziri Mhagama alienda mbali kwa kuwaombea madereva wa bodaboda kuwekewa riba nafuu katika mikopo yao na kwamba iwapo madereva wote wa bodaboda nchini watajiunga na huduma ya NMB MastaBODA, watafanikisha kasi ya pamoja kuelekea uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda.
Akisoma risala ya Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (CMPD), Michael Massawe, alisema wameupokea mfumo huu umebeba suluhu zote za changamoto za malipo na elimu ya fedha wanayokabiliana nayo. Massawe alisisitiza kuwa, katika kusaidia kundi la madereva wake kuendana na kasi ya maendeleo na mchakato wa uchumi wa kati, NMB inapaswa kukisaidia chama hicho katika upatikanaji pikipiki za mikopo ya vikundi, kwani wengi wao wanatumwa na watu.
Mkurugenzi Mkaazi wa Mastercard, Frank Molla, aliitaja
NMB MastaBODA kama njia mpya na bunifu inayoenda kumaliza changamoto za madereva na abiria wao. “Mastercard tunaamini katika matokeo chanya pale kampuni na taasisi za fedha zinapotumia teknolojia
bunifu katika kubadili maisha ya watu na kukuza uchumi
na mitaji yao kama hii inayozinduliwa leo. “Ni njia ya kisasa, shirikishi na suluhisho la changamoto za malipo yasiyohusisha pesa taslimu,' alisema.
Naye Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati wa NMB, Filbert Mponzi, alisema benki yake inajisikia furaha kushirikiana na Mastercard kuwa sehemu ya heshima na hadhi ya madereva bodaboda inayoendwa kujengwa na huduma ya NMB MastaBODA.

Alisema kuwa, uzinduzi huo wa Dar es Salaam, utafanyika katika mikoa yote inayotumia usafiri wa bodaboda, ambako wakitoka Dar watazindua Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mwanza na Dodoma, lengo likiwa ni kuwafikia madereva zaidi ya 75,000 nchini kote. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ruth Zaipuna, alikiri kushangazwa na idadi kubwa ya madereva waliojitokeza na ili kuwahamisisha katika kutumia huduma ya NMB MastaBODA, akatangaza ofa nono kwa madereva watakaofanya miamala mingi katika mwezi huu.
“Ili kuhamasisha bodaboda wengi kuingia na kuutumia
mfumo huu, natangaza ofa, madereva watano
watakaokuwa na miamala mingi kwa mwezi huu wa
kwanza, watazawadiwa bodaboda moja moja. Zawadi
zingine kama simu pamoja na kurudishiwa elfu 50 katika
miamala 50,' alisema.

No comments:
Post a Comment