Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizindua huduma ya
kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo kupitia kitengo cha Tigo Pesa
imeingia ubia na taasisi ya UmojaSwitch (BCX) imezindua huduma ya kutoa fedha
kwa njia ya ATM ambayo ni rahisi na ya uhakika kwa wateja wa kampuni hiyo
Ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ni hatua muhimu
katika kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwani inaifanya huduma
ya Tigo Pesa kuwa zaidi ya huduma ya kifedha kwa njia ya simu na kuwa huduma ya
kibenki.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema
huduma hiyo mpya ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kutoa huduma za
kidigitali zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya wateja.
“Tuna furaha kuzindua huduma hii mpya ya kibenki ambayo
itawapa wateja wetu uhuru wa kifedha kwa kuwa ni njia rahisi na ya haraka ya
kupata pesa mahali popote kupita ATM za UmojaSwitch zilizopo maeneo mbalimbali
ya nchi,” alisema Pesha.
Pesha alisema huduma hiyo mpya itarahisisha utumaji na
upokeaji wa fedha kwa kutumia ATM za UmojaSwitch zaidi ya 350 zilizopo hapa
nchini hivyo kuchochea ustawi wa kiuchumi kwa wateja wa Tigo.
“Ni matumaini yetu kuwa huduma hii itachochea utekelezaji wa
lengo letu la kuwafikia wananchi kila kona ya nchi na zaidi kuchangia agenda ya
ujumuishwaji wa watu kiuchumi.Hii inasaidiwa zaidi na mawakala zaidi ya 100,000
waliopo nchini,”alisema.
Naye, Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch, Danford Mbilinyi
alisema ushirikiano huo utachochea ukuaji wa sekta ya fedha huku ukirahisisha
upatikanaji wa huduma kwa watu wote kila mahali.
Alisema UmojaSwitch ina farijika kushirikiana na Tigo ili
kuwapatia wateja uhuru wa kifedha muda wote na zaidi kuokoa muda na gharama.
No comments:
Post a Comment