HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 23, 2019

TWARIKA YAWAMWAGIA SIFA RC KILIMANJARO NA MEYA WA MOSHI MANISPAA

Msemaji Mkuu Taasiai ya Twarika, Sheikh Haruma Husein (kushoto) na Sheikh wa Mkoa wa Kikimanjaro, Amino Mushi, wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.


Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya kiisilam ya Waviqatal Qadiriya Jailaniya Arazaqiya (TWARIKA), imemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mugwira kwa kuwaahidi kuwapatia ardhi kwa ajili ya ujenzi wa shule, hospitali na msikiti.

Aidha walimshukuru Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya (CHADEMA), aliyewapatia mabati 100 huku akiahidi mengine 150 kwa ajili ya ujenzi huo.

Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Haruna Hussein aliweleza waandishi wa habari jijini hapa mwishoni mwa wiki akiwa amembatana na shehe wa mkoa wa Kilimanjaro, Amini Mushi.

Alisema ardhi hiyo ambayo ni ekari 50 waliiomba kwa ajili ya kujenga msikiti mkubwa wa kisasa, hospitali kubwa ya mama na mtoto  na kujenga shule ya madarasa 12 kuanzia chekechekea na ukumbi wa mikutano wa kimataifa.

"Taasisi ya Twarika Tanzania ina malengo, tunajua kutafuta shilingi 100 kukusanya hadi tupate  ekari 50 ni kazi ngumu.

Tumeshaenda ofisi ya Waziri Mkuu tukafanya kikao na tumeacha barua za kuomba eneo. Tuliporudi Moshi yalipo makao makuu ya taasisi yetu, mwezi Julai (mwaka huu) na Rc (mkuu wa mkoa) alisema atatusaidia kupata  eneo hilo," alisema sheikh Haruna na kuongeza.

"Lakini kipekee nimshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond, kafanya jambo kubwa sana ambalo waislamu tunatakiwa tuige, kutoa mabati 100 kusaidia msikiti zaidi ya milioni 5. Tunamuombea Mungu akamilishe mabati 250 aliyokusudia,".

Viongozi kama hawa wanatakiwa waigwe katika jamii kwa sababu ni viongozi wanaogusa jamii inayowazunguka na hawaangalii dini Mstahiki Meya ni mkristo lakini aliguswa na akashiriki na kuamua kuwekeza mbele za Mungu,".

KONGAMANO KUBWA KUIOMBEA NCHI

Sheikh Haruna alisema kuwa wameandaa kingamano kubwa la kimataifa ambapo washiriki watatoka  Rwanda, Burundi, Kenya na wenyeji Tanzania.

Alisema kuwa kuwa kingzmani hilo litafanyika mkoani Kilimanjaro ambapo kauli mbiu yake ni 'amani ya Watanzania mwaka 2020 uchaguzi upite salama'.

"Tunahitaji uchaguzi upite salama kwa sababu Watanzania wanahitaji amani na kizazi kijacho kinahitaji amani hatuhitaji kuchafua bendera yetu ya Tanzania," alisema Sheikh Haruna.

Alisema kuwa tayari viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi za umma wamethibitisha watahudhuria akiwemo mlezi wa taasisi hiyo, Kamishina Mkuu wa shirika la Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Alan Kijazi,

 TWARIKA ILIPIGANIA UHURU
 
Sheikh Haruna alisema kuwa taasisi hiyo ilianzishwa miaka 87 uliyopita na ilishiriki katika harakati za ukombozi wa nchi hii hivyo akahimiza waislam nchini kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta amani, umoja na upendo miongoni mwa wananchi wote.

"Twarika ina miaka 87,mkoloni wakati anapigana na Nyerere (Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius)  watu waliomsaidia Nyerere kumpa nguvu kubwa walikuwa waislamu waliokiwa chini ya taasisi ya Twarika," alisema Sheikh Haruna.

No comments:

Post a Comment

Pages