HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 29, 2019

NMB YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE HUDUMA BORA


 
 Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli, akitoa huduma kwa wateja waliofika katika tawi la Msasani.
Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli, akimuhudumia mteja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja inayofikia kilele Oktoba 31, 2019.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Msasani, Halima Mcharazo, akimuhudumia mteja aliyefika tawi hapo.
Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli, akitoa huduma kwa mteja katika tawi la Msasani.

utoa hudumia wateja.
Kaimu Meneja Huduma kwa Wateja, Felister Chogo, akiwa kazini.

 Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli (kushoto), akifurahia jambo na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Msasani, Halima Mcharazo (katikati) na Baraka Mruma (kulia).
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Msasani, Halima Mcharazo (kulia), akiagana na Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli.
Mkaguzi wa Tawi Benki ya NMB, Kazumari Mfaume (kushoto), akiagana na Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli.
Ofisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Msasani wakati wa kuhitimisha Wiki ya Huduma ya Wateja.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja.

Na John Marwa

BENKI ya NMB imewataka wateja wake kuendelea kutoa ushirikiano wa kueleza changamoto, kutoa ushauri kwa Benki hiyo ili kuzidi kupata huduma bora.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 29, 2019 na Ofisa Mkuu huduma shirikishi Benki ya NMB Nenyuata Mejooli, katika kuhitimisha mwezi wa huduma kwa wateja Tawi la Msasani jijini Dar es Salaam.

Mwezi Oktoba ni mwezi wa Kibenki huduma kwa wateja, ambapo Benki hupokea na kusikiliza changamoto za wateja ili kuboresha huduma zao kila mwaka.

Amesema wateja wa NMB siku zote huwa wako karibu na Benki hiyo katika kutoa changamoto na mapendekezo ambayo yamezidi kuiimarisha Benki hiyo siku hadiz siku na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo.

"Kama inavyofahamika Oktoba ni mwezi wa huduma kwa wateja, kama NMB katika mwezi huu kuanzia Oktoba Mosi tumekuwa na mambo mbali mbali ambayo tumekuwa tukifanya kwa wateja.

"Kikubwa ambacho tumefanya ni kuongeza muda wa huduma kwa baadhi ya matawi yetu na vilevile kuwakaribu na wateja kuweza kuwasikiliza changamoto wanazozipata ni zipi, kwa sababu kutokana na changamoto wakitushirikisha inatusaidia kuweza kuboresha huduma zetu." amesema na kuongeza kuwa.

"Hivyo basi tunaomba wateja wetu watupe mrejesho ili tuweze kubadilika na kutoa huduma stahiki." alisema Mejooli
Mwezi wa huduma kwa wateja unatarajiwa kufikia tamati hapo Oktoba 30.

No comments:

Post a Comment

Pages