Siku
chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa fedha kiasi cha
Shilingi Bilioni 1.5 kwaajili ya Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na
kukagua eneo itakapojengwa hospital hiyo na kuwaekekeza JKT kuhakikisha
wanafanya kazi usiku na Mchana na kukabidhi jengo ndani ya Miezi mitatu
kuanzia leo ili wananchi wa wilaya hiyo wapate huduma Bora za Afya.
RC
Makonda amesema Hospital hiyo inajengwa eneo la Kimara Baruti kwenye
eneo lenye ukubwa wa Hekari 5.5 ambapo amemshukuru Rais Magufuli Kwa
moyo Wa Upendo anaoendelea kuonyesha kwa Wakazi wa Dar es salaam na
Wilaya ya Ubungo.
Aidha
RC Makonda amesema kuwa maandalizi yote ya ujenzi yamekamikika na kazi
ujenzi itaanza rasmi kesho huku akibainisha kuwa kukamikika kwa Hospital
hiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza changamoto za Afya Wilayani
humo.
Itakumbukwa Juzi
October 26 wakati wa hafla ya Kupokea ndege ya 8 Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda alitumia hafla hiyo kuwasilisha kilio cha
wakazi wa Ubungo juu ya kukosekana kwa hospital ya wilaya ya Ubungo
ambapo Rais Magufuli alipokea kwa mikono miwili ombi hilo na Kumuelekeza
Waziri wa TAMISEMI kutoa fedha hizo na hatimae leo utekelezaji wa
ujenzi unaanza.
No comments:
Post a Comment