Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Amana, Dk. Muhsin Masoud, akizungumza na wateja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu y a Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi. (Picha na Suleiman Msuya).
Na Suleiman Msuya
BENKI ya Amana katika kupanua huduma zake imeanzisha huduma ya kutoa ada ili kutua mzigo huo kwa wazazi na walezi.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dk. Muhsin Masoud, wakati wa hafla
ya kusherehekea miaka nane ya Amana Benki iliyofanyika jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Dk.
Masoud alisema elimu ni jambo la muhimu katika jamii hivyo wanaamini
huduma hiyo itaweza kusaidia wazazi na walezi ambao wanakumbana na
changamoto ya kulipa ada.
Mkurugenzi huyo alisema utaratibu wa kutoa mkopo wa ada utahitaji masharti madogo ikiwemo shule anayosomea mtoto kumdhamini.
“Amana
Benki ni benki ya wananchi tumekuja na huduma katika wiki ya huduma kwa
wateja tukiamini jamii itanufaika kwa kupata mkopo wa ada ili
kulipia watoto wao hivyo kumuondolea mzazi hofu ya kupata ada.
Utaratibu wa kurejesha ada hiyo utakuwa wa mwaka mmoja na kama mzazi atahitaji kuongeza mkopo tutajadiliana upya,” alisema.
Alisema
“Kaulimbiu ya wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu ilikua ni ‘Tabasamu
lako, Furaha yetu’ ikiwa ni kiashiria katika uhamasishaji wakiutendaji
na ubunifu wa suluhu mbalimbali zinazopelekea kuwarahisishia wateja
katika upataji wa huduma za kifedha ambazo zinakidhi mahitaji ya Watanzania wakipato cha kati na chini.
Mkurugenzi
huyo alisema mikopo yao inalenga watu wanye mahitaji ya mikopo midogo
ya biashara, elimu na vikundi (Solidarity Group Financing) kwa lengo la
kuwakomboa kiuchumi”.
Alisema
katika kuadhimisha wiki hiyo Amana Benki inaendelea kuwaelimisha wazazi
na walezi juu ya uwezeshwaji unaofanywa hasa katika masuala ya elimu
wameamua kutoa mkopo wenye lengo la kupunguza mzigo wa ada za shule.
"Amana Benki inaendelea kukua, na jitihada za kufikisha huduma zake maeneo mbalimbali ya Tanzania
zinaendelea mwaka huu imefanikiwa kufungua tawi la tisa (9) Zanzibar na
maandalizi yakufungua tawi lake la 10 mkoani Dodoma mwaka 2020
yanaendela," alisema.
Pia,
alisema benki hiyo kwa sasa ina mawakala zaidi ya 400 maeneo mbalimbali
katika kurahisisha upatikanaji wa baadhi ya huduma zake.
Dk.
Masoud alisema dira ya Amana Benki ni kuwa chaguo la kwanza na kiongozi
katika utoaji huduma za kibenki zinazozingatia misingi ya kiislam.
"Dira
hii inafuatiwa na dhamira ya kutoa huduma za kisasa na za kipekee kwa
kuzingatia maadili kwa njia iliyowazi kwa kupitia teknolojia za kisasa,"
alisema.
Mkuu wa idara
ya Masoko, Dassu Mussa, alisema sambamba na kauli mbiu ya “Tabasamulako,
Furahayetu” Amana Benki, imeendeleza jitihada za kuongeza uwezo kwa
wateja kuweza kupata huduma kiurahisi na kuwa miongoni mwa benki
itakayozindua mfumo wakidigitali utakaofahamika kama Amana Benki Mobile
App maalum kwa watumiaji wa simu janja.
"Mfumo huu utazidi kuwarahishia wateja katika kupata huduma za kibenki kupitia simu zao na kwa gharama nafuu zaidi” alisema.
No comments:
Post a Comment