Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa, jana akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) jimbo la Arusha Mjini, Ephata Nanyaro, akiwa ameambatana na viongozi wengine. (Picha zote na Grace Macha).
Balozi
wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa, akikumbatiana na Kaka
yake Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) ,
Tundu Lissu, Alute Mugway, mara baada ya ibada ya mazishi ya baba yake Dk.
Slaa, Peter Tluway (105).
NA GRACE MACHA, ARUSHA
BABA
wa balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk. Wilbrod Slaa, Peter Tluway
(105) anayetarajiwa kuzikwa Novemba 23, 2019 nyumbani kwake, Ayalabe, Karatu.
Leo
imefanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu nyumbani kwa mtoto wake,
kata ya Sokon 1 jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro na Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia, (Chadema) wilayani Arusha, Ephata Nanyaro.
Mjukuu
wa marehemu, Emiliana Willbrod, akisoma historia fupi alisema kuwa babu
yao,mzee Tluwey alifariki novemba 18, mwaka huu kutokana na matatizo ya
moyo na umri mkubwa yaliyokiwa yakimsumbua.
Alisema babu yao alizaliwa mwaka 1914 na alikuwa akizungumza lugha tatu Kiiraq, Kiswahili na Kiingereza.
Emiliana
alisema kuwa babu yao alikuwa mpishi mzuri kwenye nyumba za kikoloni
baadaye akawa mpishi kwenye hoteli za kitalii kwenye miji ya Arusha na
Karatu pamoja na kujishughulisha na ufugaji.
Alisema
kuwa babu yao alianza kuugua 2011 akisumbuliwa na moyo lakini pia na
magonjwa mengine yaliyosababishwa na umri wake mkubwa.
"Aprili
7, mwaka huu familia yetu ilitikiswa, babu alipata stroke akiwa Karatu,
akaaga dunia Novemba 18, mwaka huu," alisema mjukuu wa babu huyo
akisoma historia fupi ya marehemu na kuongeza.
"Alikuwa na mke ambaye ni bibi yetu, Emiliana Enezeti waliyefunga ndoa 1947 na alifariki 2001,"
Mjukuu
huyo alisema kuwa wakati wa uhai wao bibi na babu yao walijaliwa kupata
watoto watatu wa kiume ingawa mmoja alifari hivyo marehemu ameacha
watoto wawili, Wajukuu 12 na vitukuu 11,".
Akitoa
salama za rambirambi, Mwenyekiti wa Bawacha jimbo la Arusha Mjini,
Prisca Kinabo, ambaye aliwapa pole wanafamilia huku akihimiza upendo
miongoni mwao.
Alisema
kuwa wamemsindikiza diwani wao wa viti maalum, Sabina Fansis ambaye ni
mke wa mdogo wake Dk. Slaa, marehemu, Fransis Peter.
No comments:
Post a Comment