November 30, 2019

DK. KIGWANGALLA AZINDUA HIFADHI ZA IBANDA NA RUMANYIKA MKOANI KAGERA

Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akihutumia katika uzinduzi wa hifadhi za Taifa za Ibanda na Rumanyika zilizopo mkoani Kagera.


Alodia Dominick, Kyerwa

Waziri wa Mali Asili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amesema kama wananchi wanaozunguka hifadhi za wanyama pori hawatazilinda serikali itatumia askari wa mapori kuzilinda.

Ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa hifadhi za wanyama pori mbili za Ibanda iliyopo wilaya ya Kyerwa na Rumanyika iliyopo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Katika hotuba ya uzinduzi wa hifadhi hizo uliofanyika katika hifadhi ya wanyama pori ya Ibanda, waziri Kigwangalla amesema iwapo wananchi wanaozunguka hifadhi hizo hawatahiari kuzilinda serikali itatumia maaskari wake kuzilinda wenyewe.

"Ni jukumu la kila mtanzania kulinda na kuhifadhi mazingira kama wananchi hawatahiari kuyalinda basi serikali italinda mazingira ya hifadhi hizo kwa kutumia maaskari wake" Amesema waziri Kigwangara.

Ameongeza kuwa, hifadhi za Ibanda na Rumanyika zina historia ya kipekee ambapo amesema, Hifadhi ya Rumanyika alikuwa anaishi mkama Rumanyika na hifadhi ya Ibanda ni eneo ambalo mkama Rumanyika alilitumia kama sehemu ya kwenda Kupumzika.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Hifadhi za wanyama pori Tanzania TANAPA, Allan Kijazi, amesema kuwa wameanza ujenzi wa hotel ya kulaza wageni 50 katika hifadhi ya Burigi Chato, inajengwa hostel ya vitanda 80 vyenye gharama nafuu kwa ajiri ya watalii wa ndani hifadhi za Ibanda na Rumanyika.

Ameongeza Ibanda na Rumanyika wamepandikiza kundi la simba kutoka Burigi wataongeza faru weupe na weusi hifadhi ya Burigi na katika hifadhi ya Rumanyika wataongeza golira na chimpanzee.

Kijazi amesema  kuwa, watashirikiana na uongozi wa wilaya Kyerwa kufungua uwanja wa ndege utakaotumiwa na watalii nia ni kuhakikisha wanaunganisha utalii kutoka Serengeti,Rubondo, kisiwa cha saa nane hadi Ibanda.

Naye wakala wa huduma za utalii Wilberdi Chamburo amewataka wanakagera kutoogopa kuthubutu katika biashara na kwamba wawekeze kwenye utalii ili wapende mali zao za asili.

Pia mbunge wa jimbo la Kyerwa Innocent Birakwate amewaomba TANAPA kutoa elimu kwa wananchi ili wanyama, wananchi na wahifadhi wawe kitu kimoja na kuwa wana Kagera na Kyerwa waitumie nafasi kuwekeza wawekezaji wasitoke nje ya mkoa na wilaya na mwisho ameomba iwepo miundo mbinu bora kwa ajili ya watalii kufika kirahisi.

No comments:

Post a Comment

Pages