November 30, 2019

WANAFUNZI WANAOKWENDA NJE YA NCHI WAASWA KUZINGATIA KINACHOWAPELEKA NJE YA MIPAKA YA TANZANIA


 Meneja Uendeshaji Taasisi ya Vyuo Vikuu vya nje Tanzania 'University Abroad', Rachel Mansuli, akizungumza na mmoja kati ya wanafunzi 15 waliokwenda nchini Chini kusomea masomo ya udaktari, Sarah Phiri, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Novemba 28, 2019.
 Meneja Uendeshaji Taasisi ya Vyuo Vikuu vya nje Tanzania 'University Abroad', Rachel Mansuli, akizungumza na mmoja kati ya wanafunzi 15 waliokwenda nchini Chini kusomea masomo ya udaktari, Sarah Phiri, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Novemba 28, 2019.

Wanafunzi wanaokwenda kusoma masomo mbalimbali nchini China wakipitia taarifa zao kabla ya kuanza safari yaoNovemba 28, 2019.

Na Mwandishi Wetu 

MENEJA Uendeshaji Taasisi ya Vyuo Vikuu vya nje Tanzania 'University Abroad' Rachel Mansuli amewataka wanafunzi wanaokwenda kusoma nje kuzingatia kilichowapeleka ili waweze kurejea na ujuzi wa kulisaidia Taifa. 

Ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga wanafunzi 15 walioelekea nchini China kwa ajili ya masomo katika kozi mbalimbali. 

Rachel amesema kundi hilo la wanafunzi 15 kuna wanaokwenda kusomea Udaktari,  Urubani pamoja na Uchumi na Biashara. 

"Matarajio yetu ni kuona vijana hawa wanakwenda kupata ujuzi ambao watarudi hapa  nyumbani kuja kushirikiana na wataalamu wengi ili kuweza kuisadiaa nchi yetu kupiga hatua.

"Wamo madaktari ambao tunaamini elimu wanayoenda kuipata itawapa uwezo wa kuja kujenga taifa letu, vivyo hivyo kwa Wahandisi  na Wachumi wa Biashara. 

"Kikubwa tunawasihi na kuwaomba wakafanye kinachowafanya kuziacha familia zao na taifa lao ili baadae warejee kutoa mchango wao kwa nchi yetu".

Baadhi ya Wanafunzi ambao wameondoka wametoa shukrani zao kwa taasisi hiyo na familia zao kwa kuwawezesha kuanza safari ya kutimiza ndoto zao. 

"Natambua nchi yetu ina ombwe kubwa la wataaalamu wa Afya, hivyo basi mapenzi yangu ya kuwa daktari ni sehemu ya kwenda kupata ujuzi ili nije kutoa mchango wangu kwenye Taifa langu ". amesema Sara Phiri mwanafunzi wa Udaktari. 

"Nimechagua kwenda kusoma nje ili nikapate ujuzi wa juu zaidi katika fani hii ya Uinjinia kwani bado kama nchi tunahitaji wataaalamu wengi hasa katika kuelekea Tanzania ya Viwanda "amesema Bernard Swara anenda kusomea Uinjinia.

"Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa University Abroad kuwa sehemu ya kufanikisha safari ya kutimiza ndoto zetu ili tuweze kupata maarifa na ujuzi wa kuja kurijenga Taifa letu ".amesema Everest Munish mwaanafunzi wa Uchumi na Biashara. 

Hii ni awamu ya tano kwa University Abroad kupeleka wanafunzi katika mataifa mbali mbali mwaka huu ambapo wanatarajia kuwa na awamu nyingine mbili kabla ya mwaka kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Pages