HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2019

JAMII YATAKIWA KUFAHAMU MATUMIZI SAHIHI YA ANTIBIOTIKI

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Eliasi Kwesi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.


Na Asha Mwakyonde

JAMII imetakiwa  kuelewa athari na tatizo kubwa ambalo limekuwa likiongezeka duniani kote litokanalo na usugu wa vimelea dhidi ya dawa za Antibiotiki.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam Novemba 15, 2019 na  Kaimu  Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Eliasi Kwesi, wakati akizindua rasmi  shughuli za kuhamasisha matumizi sahihi  ya dawa za Antibiotiki katika kuelekia wiki ya
Antibiotiki  duniani itakayofanyika kuanzia Novemba 18-24, mwaka huu duniani kote.

 Dk. Kwesi amesema kuwa lengo ni kusisitiza na kuongeza uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa hizo ili kupunguza matumizi yasiyostahili na hatimaye kuzuia ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa  za Antibiotiki.

"Serikali imendaa mipango na miongozo mbalimbali ili kutekeleza kazi kwa usahihi ikiwa ni pamoja na mpango wa Taifa wa kupambana na usugu wa dawa dhidi ya vimelea mbalimbali Antimicrobial ( 2017-2022)., " amesema Dk. Kwesi.

Amefafanua kuwa ripoti ya  benki ya Dunia ya mwaka 2017 inabainisha kwamba  watu zaidi  ya 700,000 wanafariki kila mwaka kutokana na usugu  wa dawa za Antibiotiki.

Dk.Kwesi  amewaagiza   watoa  huduma za dawa  nchini kuandika  dawa kwa kufuata mwongozo  wa matibabu wa mwaka 2017 na kutumia majina halisi ya dawa (Generics).

Nao wadau walioshiriki katika tukio hilo wakiwemo wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya (WHO), Shirika la Chakula (FAO) na Shirika la Wanyama (OIE) wamesema wanashirikiana kwa pamoja na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya tatizo hilo.

Uznduzi huo umehudhuriwa na kamati ya kitaifa  ya uratibu na udhibiti wa usugu wa  vimelea dhidi ya dawa katika wiki ya uhamasishaji wa matumizi sahihi ya Antibiotiki nchini

No comments:

Post a Comment

Pages