Wafungaji wa mabao mawili yaliyoipa ushindi timu ya Taifa
ya Tanzania 'Taifa Stars', dhidi ya Guinea ya Ikweta, Salum Aboubakar
'Sure Boy' na Saimon Msuva, wakishangilia bao la pili lililofungwa na
Sure Boy katika dakika ya 90 ya pambano la kuwania kufuzu AFCON 2021
uliofanyika Novemba 15, 2019 kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam. Stars ilishinda 2-1.
(Picha na Francis Dande).
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ’Taifa Stars’, Mbwana Samatta,
akimtoka beki wa Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON)
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' wakishangilia timu
yao ilipopambana na Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ’Taifa Stars’, Mbwana Samatta,
akimtoka beki wa Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON)
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Golikipa wa timu ya Taifa ya
Guinea ya Ikweta akiokoa mkwaju uliopigwa na mshambuliaji wa timu ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta, katika mchezo wa kuwania
kufuzu finali za Mataifa ya Afrika (AFCON) uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Guinea ya Ikweta,
Felipe Ovono Ovono, akijaribu bila mafanikio kuokoa kombora lililopigwa
na kiungo, Salum Aboubakar 'Sure Boy', lililotinga kimiani kama
linavyoonekana na kuipa Taifa Stars bao la pili na la ushindi, katika
mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021),
iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Na John Marwa
TIMU
ya Taifa, Taifa Stars imeanza vyema kampeni ya kuwania kufuzu fainali
za Mataifa ya Afrika AFCON 2021 kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
dhidi Equatorial Guinea mchezo wa kwanza hatua ya makundi.
Ulikuwa mchezo wa ufunguzi wa kundi J lenye timu za Libya, Tunisia, Equatorial Guinea pamoja na Tanzania.
Mchezo
huo uliolindima katika Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2019, Stars walikubali
kutanguliwa kwa kuruhusu bao kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo
Pedro Obiang dakika ya 14 ya mchezo.
Hadi
mapumziko Stars ilikuwa nyuma kwa bao moja kwa bila huku ikiwa
imepoteza nafasi za wazi katika kipindi hicho kupitia Nahodha Mbwana
Samatta na Simon Msuva.
Kipindi
cha pili Stars walirejea kwa kasi kusaka kusawazisha bao, ambapo juhudi
za winga teleza Simon Msuva zilimuwezesha kuisawazishia Stars dakika ya
68 ya mtanange huo.
Wakati
mtanange huo ukielekea ukingoni Abubakar Salum 'Sure Boy' akipachika
bao la pili na la ushindi dakika ya 90 ya mchezo kwa bonge la shuti na
kuiwezesha Stars kuvuna pointi tatu za nyumbani.
Stars
inahitaji kufanya vema katika hatua hiyo ya makundi ili iweze kufuzu
tena kwa mara ya pili mtawalia baada ya kufanya hivyo fainali zilizopita
zilizofanyika nchini Misri mwaka huu.
Stars inatarajia kuondoka kesho kuelekea Tunisia kuwakabili Libya katika mchezo wa pili wa kundi J la mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment