November 18, 2019

STEFANOS TSITSIPAS BINGWA ATP, AVUNJA REKODI YA MIAKA 18

Stefanos Tsitsipa.
 Stefanos Tsitsipas wa Ugiriki akipozi na taji la ATP Finals alilotwaa Jumapili jioni.


LONDON, UINGEREZA
 
NYOTA wa tenisi, Stefanos Tsitsipas jana Jumapili ameandika rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi katika kipindi cha miaka 18 kutwaa taji la ATP Finals 2019, baada ya kumchapa Dominic Thiem kwenye Uwanja wa 02 Arena, huku akiweka wazi siri ya ushindi wake.

Tsitsipas, raia wa Ugiriki mwenye umri w mikaa 21, alitoka nyuma baada ya kupoteza seti ya kwanza, hatimaye akapambana na kuibuka na ushindi wa 6-7 (6-8) 6-2 7-6 (7-4) na kutwaa taji hilo kubwa zaidi katika maisha yake ya kucheza tenisi.

Kwa ushindi wa juzi jioni, Tsitsipas anakuwa bingwa mwenye umri mdogo zaidi kutwaa ATP, tangu nyota wa kimataifa wa Australia, Lleyton Hewitt aliyefanya hivyo mwaka 2001. Mgiriki huyo amezawadiwa kiasi cha pauni milioni 2 kwa kutwaa taji hilo.

"Kushika taji hili ilikuwa ni ndoto yangu, nashukuru imekuwa kweli hatimaye. Nilikuwa Napata wakati mgumu baadhi ya vipindi mchezoni, lakini nilichagua kuyasahau na kupambana na hatimaye kufikia malengo.

"Siri ya mafanikio yangu ni hamasa ya kupambana bila kuchoka wala kukata tamaa, lakini pia kujilazimisha kujisukuma katika kufanya kilicho bora na mwisho wa siku kumaliza mchezo nikiwa mshindi," alisema.

Tsitsipas pia ameweka rekodi ya kuwa kijana mdogo aliyetwaa taji katika fainali yake ya kwanza tangu John McEnroe alipofanya hivyo mwaka 1978.

BBC Sport

No comments:

Post a Comment

Pages