HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 18, 2019

KOCHA AFUKUZWA KAZI ITALIA KWA SABABU YA KUSHINDA BAO 27-0

Kikosi cha Invicta Sauro FC kikiwa katika picha ya pamoja na kocha wao aliyetimuliwa kazi wa kwanza kushoto.
MILAN, ITALIA

HISTORIA imeandikwa, baada ya juzi Jumamosi kocha Massimiliano Riccini kufutwa kazi nchini Italia baada ya kuiongoza timu yake Invicta Sauro FC kushinda mabao 27-0 dhidi ya ya Marina Calcio katika Michuano ya Ligi ya Vijana, sababu ikitajwa kuwa ni udhalilishaji.

Rais wa Invicta Sauro FC ya Grosseto mjini Tuscany, Paolo Brogelli, amesema ushindi huo dhidi ya Marina Calcio ni wa udhalilishaji na haukuwa na lengo la kuwafunza watoto wa timu iliyoshindwa wala iliyoshinda, hivyo uongozi wa timu umeamua kumfuta kazi kocha huyo. 

“Wapinzani wetu lazima waheshimiwe, mimi kama Rais wa timu kuna vitu sijaviona uwanjani leo. Kufunga mabao mengi ni udhalilishaji, mbali na mabao, nilitegemea kuona watoto wanaelimishwa zaidi uwanjani kuliko kufunga.

“Hicho kitu leo sijakiona, makocha wanatakiwa kuwafundisha wachezaji hususani watoto wao nidhamu na kuheshimu wapinzani,” alisema Brogelli kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Hii sio mara ya kwanza kocha kutimuliwa kazi kutokana na aina hiyo ya matokeo, kwani mwaka 2015, Serranos Sub 11 ya Hispania iliichapa Benicalap FC kwa mabao 25-0, matokeo yaliyomfukuzisha kazi kocha wa Serranos, Pau Cercos, kwa kilichoitwa kukosea heshima timu pinzani.

No comments:

Post a Comment

Pages