HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 15, 2019

Kongamano la Utafiti na Maendeleo Endelevu lazinduliwa jijini Dodoma


 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Pili la Utafiti na Maendeleo Endelevu la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Jijini Dodoma. 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia Kongamano.
 Balozi wa Sweeden Tanzania Anders Sjoberg akizungumza na washiriki wa kongamano la Pili la Utafiti na Maendeleo Endelevu lilizunduliwa leo Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, akipata maelezo ya utengenezaji wa Juisi ya Ndizi kwa njia ya kisasa kutoka kwa Dkt. Oscar Kibazohi (Kulia) wa UDSM baada ya uzinduzi wa Kongamano. (Picha na Francisca Swai).

Na Francisca Swai
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amezindua rasmi kongamano la pili la Utafiti na maendeleo ya Endelevu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Serikali ya Sweeden kupitia mradi wa SIDA/ SAREC.
Kongamano hilo la siku mbili kuanzia tarehe 14 na 15 Novemba,2019  limefanyika Jijini Dodoma.
Kongamano hilo, limewashirikisha wanataaluma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikisha wanataaluma kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi, wadau wa maendeleo, wawakilishi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la Wawakilishi kutoka Zanzibar, Asasi za Kijamii, Wizara na Taasisi mbalimbali.  
Lengo la Kongamano hilo ni kuzungumzia utekelezaji wa mpango wa SIDA   inayotekelezwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kipindi cha Miaka mitano 2015 – 2020, miongoni mwa tafiti zitakazo jadiliwa ni pamoja na Kilimo-Biashara, Utalii, Usalama wa Chakula, Sayansi ya Bahari na tafiti mbalimbali zenye kugusa maendeleo ya wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages