Na Suleiman Msuya
WASAYANSI watafiti wanaoshiriki
mkutano wa mwaka wa Baraza la Sayansi Kanda ya Afrika wamezitaka nchi zao,
kuhakikisha zinakuwa na Sheria na Sera ambazo zitawezesha wanawake watalaam
kushiriki katika utafiti ili kuwepo usawa wa kijinsia.
Hayo yamsemwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Utafiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Prof.
Mohammed Sheikh (pichani), wakati akitoa taarifa ya mkutano huo ambao unaisha leo Novemba 15, 2019.
Prof. Sheikh alisema
takwimu zinaonesha uwiano kati ya wanaume na wanawake kwenye kufanya utafiti
haulingani hivyo Serikali za Afrika zinapaswa kuweka mfumo ambao utarahisha
usawa kisheria na kisera.
"Tumejadiliana na
asilimia kubwa hoja ya ushiriki wa wanawake katika utafiti imechukua nafasi
kubwa kwani takwimu zinaonesha karibu nchi zote ushiriki upo chini hivyo njia
rahisi ni kuwepo mifumo ya kisheria na kisera ambayo itapendelea kundi la
wanawake.
Ili kufikia huko ni muhimu taasisi za utafiti
zinakuwa na ushirikiano kikazi kwa kuwawezesha wanawake wanasayansi kufanya
utafiti kama walivyo wanaume," alisema.
Sheikh alisema
wasayansi hao wanaamini iwapo kundi hilo litapewa msukumo dhana ya usawa wa
kijinsi itaonekana na kuondoa malalamiko.
Aidha, alisema wanataaluma
hao wamejadili namna ya kuwawezesha watafiti wanaoibukia fedha za kufanyia
utafiti ili iwe rahisi kuwaingiza kwenye mfumo kitafiti ulio bora.
Alisema Tanzania
kupitia COSTECH na nchi ya Sweden imekuwa ikiwezesha watafiti wanaochipukia
kuanzia mwaka 2015 programu ambayo imeonesha matokeo chanya.
"Karibu Euro
900,000 zimeweza kutumika kuwezesha watafiti wapya hivyo ni jukumu la wenzetu
kuchukua mfumo huu na kuupeleka kwao,” alisema
Aidham alisema kupitia mkutano
wamekutana na Baraza la Utafiti la Norway na kubadilishana uzoefu katika
shughuli za utafiti.
Mtafiti kutoka Taasisi
ya Taifa ya Sayansi nchini Marekani, Makyba Charles alisema nchini kwao
wamekuwa wakizingatia jinsia kwenye utafiti kwa kuwepo vipengele vya sheria na
sera.
Charles alisema nchini
Marekani sheria na sera zinaelekeza taasisi za utafiti kuzingatia usawa wa
kijinsi hivyo ameshauri nchi za Afrika kuzingatia hilo.
Alisema nchini Marekani
iwapo kutatokea unyanyasaji wa kijinsia sheria zinaelekeza tukio hilo
liripotiwe ndani ya siku 10 ili hatua zichukuliwe.
Mtafiti Mwandamizi wa
COSTECH, Hildegalda Mushi alisema washiriki wamependekeza changamoto zote
ambazo zinarudisha nyuma watafiti wanawake zipatiwe ufumbuzi.
"Muda mwingi ulitumika
kujadili namna ya kuwezesha kundi letu la wanawake kuhakikisha linaambukizwa
chachu ya kufanya utafiti kama walivyo wanaume," alisema.
Alisema washiriki
walisema ili kundi hilo liweze kuwa shindani linahitaji kujengewa uwezo kuanzia
elimu ya msingi hadi vyuoni ambapo takwimu zinaonesha ushiriki wao umeshuka.
Mushi alisema pia
wamekubaliana kila nchi shiriki kukusanya takwimu za ushiriki wanawake kwenye
utafiti ili kuwa na taarifa sahihi.
Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Teknolojia, Sera na Ubunifu Afrika (ATPS), Nicholas Ozor alisema
pamoja na uwezeshwaji wanawake na watafiti wanaochipukia juhudi kubwa zinapaswa
kuelekezwa kwenye utafiti ulio wazi.
Ozor alisema ulimwengu
wa leo unahitaji ushirikiano katika kila
jambo hivyo iwapo mfumo wa utafiti wa kisayansi uliowazi ukipata nafasi
kutakuwa na matokeo chanya.
"Sisi ATPS
tunaamini katika utafiti uliowazi kama njia ya kuendeleza jinsia na watafiti
wanaochipukia tunachopigania ni uwepo wa miundombinu rafiki katika kitekeleza
adhma hiyo," alisema.
No comments:
Post a Comment