Harry Kane. |
Mourinho. |
LONDON, UINGEREZA
MRENO
Jose Mourinho ameandika rekodi mpya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
(UCL), baada ya usiku wa kuamkia jana kuiongoza Tottenham Hotspur ya London,
Uingereza kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na hatimaye kushinda kwa mabao 4-2.
Tottenham
ilikuwa nyumbani jijini London, ambako iliibua hofu kwa mashabiki baada ya
kukubali kipigo cha mabao mawili ndani ya dakika 20 kwanza kutoka kwa wageni
wao Olympiacos ya Ugiriki. Mabao hayo yalifungwa na Youssef El Arabi na Ruben
Semedo.
Mourinho
akapata nafuu baada ya Dele Alli na Harry Kane kuisawazishia mabao hayo kunaako
dakika za 45 na 50, kabla ya Serge Aurier kuipa bao la uongozi Tottenham dakika
ya 73 na baadaye Kane kufunga bao la nne dakika ya 77.
Kwa
mabao hayo, Mourinho ameingia katika vitabu vya kushinda kwa mara ya kwanza
mechi aliyotoka nyuma kwa mabao 2-0 katika historia yake kwenye michuano ya
UCL, ambayo ametwaa taji mara mbili akiwa na timu za FC Porto ya Ureno (2004) na
Inter Milan ya Italia (2010).
MATOKEO LGI YA MABINGWA ULAYA JANA
USIKU
KUNDI A
Galatasaray
1-1 Club Brugge
Real
Madrid 2–2 PSG
KUNDI B
Crvena
Zvezda 0-6 Bayern
Tottenham
4-2 Olympiacos
KUNDI C
Atalanta
2-0 Dinamo Zagreb
Man
City 1-1 Shakhtar Donetsk
KUNDI D
Lok.
Moscow 0-2 Leverkusen
Juventus
1-0 Atletico Madrid
Daily
Mail
No comments:
Post a Comment