HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 27, 2019

Jurgen Klinsmann kocha mpya Hertha Berlin

Jurgen Klinsmann 

MUNICH, UJERUMANI

KOCHA wa zamani wa timu za taifa za Ujerumani na Marekani, Jurgen Klinsmann, ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya Hertha Berlin kwa mkataba mfupi hadi mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga.’

Berlin haina kocha baada ya kumfukuza kocha Ante Covic na sasa inamtangaza mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham, Inter Milan na Bayern Munich mwenye umri wa miaka 55, ambaye anatangazwa kuwa msimamizi kuelekea mwisho wa msimu.

Covic, 44, ametimuliwa kazi Julai mwaka huu, ambako ameiongoza timu kupata matokeo mabaya tangu mwanzo wa msimu hadi sasa inaposhika nafasi ya 15 katika Bundesliga, ligi inayoshirikisha timu 16.

Kibarua cha awali kwa Klinsmann akiwa kocha wa Berlin, kitakuwa Jumamosi hii wakati kikosi chake kitakapokuwa nyumbani kuwaalika Borussia Dortmund.

BBC Sport

No comments:

Post a Comment

Pages