HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 28, 2019

SBL yahimiza mfumo kodi ya pamoja EAC

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti, Mark Ocitti (wa pili kulia), akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushuru na Biashara wa Sekretariati ya EAC, Kenneth Bagamuhunda. (Na Mpiga Picha Wetu).


Na Mwandishi Wetu, Arusha

 
KURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, ameshauri kuharakishwa kwa utaratibu wa kuoanisha mfumo wa kodi kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Ocitti amesema, pamoja na kwamba hatua nzuri na kubwa imefikiwa, vikwazo vya kibiashara vilivyopo havina budi kushughulikiwa kuongeza kasi ya uwekezaji pamoja na kurahisisha biashara ya bidhaa na huduma miongoni mwa nchi wanachama.

Akizungumza katika mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Wakuu wa Nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, Ocitti alisema tafsiri tofauti za vipengele vya kisheria kama ‘bidhaa  za nje’ imesabisha kuwepo kwa kodi kubwa kwa bidhaa zinazotoka ndani ya nchi wanachama jambo ambalo limepunguza kasi ya ukuaji wa biashara.

“Utekelezaji wa kuoanisha mfumo wa kodi miongoni mwa nchi wanachama umekuwa hauendi vizuri sana kwa sababu mbalimbali ikiwamo utofauti wa kiuchumi na kufikiria suala la mapato, viwanda vya ndani, ushindani na nyinginezo,’ alisema.

Akizungumzia athari zake kwenye sekta ya uzalishaji wa bia, alisemautofautiwakodi za ndani miongoni mwa nchi wanachama, umesababisha kuongezeka kwa pombe haramu na kuongeza kiwi bado kuna changamoto katika utekelezaji wa kanuni itayoweka mfumo wa kodi unaofana na kutokana na utofauti wa maendeleo ya kiuchumi, pia hakuna msukumo wa kisheria unatoa msisitizo kwa jambohilo.

“Kasi ndogo ya upitiaji wa Itifaki ya Ushuru wa Forodha kwa nchi wanachama wa EAC unaathiri baadhi ya shughuli kuzifanya bajeti za nchi hizi kutegemea kwa kiasi kikubwa ushuru wa forodha. 

Hata hivyo, kuanzia mwaka 218 kumekuwa na mfumo mzuri kati ya nchi wanachama kwa kukulia na muundo wa 0%, 10%, 25% na 35.

Akizungumzia namna kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) ambayo ni kampuni mama ya SBL ilivyoathirika, alisema imekuwa ni bahati nzuri kiwi makampuni yaliyochini ya EABL yamesajiliwa kama makapuni ya ndani kwa nchi wanachama.

Hivyo hayajaathirika sana kwa kiwi bidha azakezinazalishwandaniyanchihizo.

“Hatahivyo, uwekaji wa viwango vya pamoja bidhaa ambazo zipo tayari kwa ajili ya kutumika (RTD) imeleta shida kwa mfano kwenye biashara ya bidhaa hizo zinazotoka Kenya kuja Tanzania,” alisema

No comments:

Post a Comment

Pages