Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magessa
(kulia) akitoa ufafanuzi jana wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha
Baraza la Madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji wa Nzega William Jomanga (katikati) akisitiza jambo wakati
akifungua jana kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani. (Picha na Tiganya Vincent).
Na Tiganya Vincent
MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Nzega wameshauriwa
kuhakikisha kila Shule katika Kata zao inakuwa na mashamba darasa kwa ajili ya
uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo ya chakula.
Hatua itaziwezesha Shule kuwa na chakula
ambacho kitatumiwa na wanafunzi na hivyo kuongeza usikivu wawapo kwenye masomo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo William Jomanga wakati akifungua kikao cha robo ya kwanza ya
Baraza la Madiwani.
Alisema pamoja na kuwasahauri wazazi wajenge
desturi ya kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao mashuleni ili kuongeza
kiwango cha ufaulu pia ni kila shule iwe na shamba la mfano kwa ajili ya
uzalishaji wa chakula cha wenyewe.
Jomanga alisema kuwa zipo shule zina mashamba
ni vema wakatumia maeneo hayo kulima mashamba ya mfano ambayo yatawapa chakula
na wananchi watakwenda pale kujifunza.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mteandaji wa
Halmashauri ya Nze Mji Philemon Magesa alisema ufaulu wa wanafunzi unategemea
ushirikiano baina ya wazazi , walimu na jamii ikiwemo kuhakikisha watoto
wanapata chakula cha mchana.
Alisema wakitambua kuwa watoto wanahitaji
chakula cha mchana shule watachangia kwa kuzingatia utaratibu ambao watakubaliana
na kuwaweza watoto wao kupata mlo wa mchana na hivyo kuwaongezea utulivu.
No comments:
Post a Comment