Stefanos Tsitsipa.
Stefanos Tsitsipas wa Ugiriki akipozi na taji la ATP Finals alilotwaa Jumapili jioni.
LONDON,
UINGEREZA
NYOTA wa tenisi, Stefanos Tsitsipas jana Jumapili ameandika rekodi
ya kuwa mchezaji mdogo zaidi katika kipindi cha miaka 18 kutwaa taji la ATP
Finals 2019, baada ya kumchapa Dominic Thiem kwenye Uwanja wa 02 Arena, huku
akiweka wazi siri ya ushindi wake.
Tsitsipas, raia wa Ugiriki mwenye umri w mikaa 21,
alitoka nyuma baada ya kupoteza seti ya kwanza, hatimaye akapambana na kuibuka
na ushindi wa 6-7 (6-8) 6-2 7-6 (7-4) na kutwaa taji hilo kubwa zaidi katika
maisha yake ya kucheza tenisi.
Kwa ushindi wa juzi jioni, Tsitsipas anakuwa bingwa
mwenye umri mdogo zaidi kutwaa ATP, tangu nyota wa kimataifa wa Australia,
Lleyton Hewitt aliyefanya hivyo mwaka 2001. Mgiriki huyo amezawadiwa kiasi cha
pauni milioni 2 kwa kutwaa taji hilo.
"Kushika taji hili ilikuwa ni ndoto yangu,
nashukuru imekuwa kweli hatimaye. Nilikuwa Napata wakati mgumu baadhi ya
vipindi mchezoni, lakini nilichagua kuyasahau na kupambana na hatimaye kufikia
malengo.
"Siri ya mafanikio yangu ni hamasa ya kupambana
bila kuchoka wala kukata tamaa, lakini pia kujilazimisha kujisukuma katika
kufanya kilicho bora na mwisho wa siku kumaliza mchezo nikiwa mshindi,"
alisema.
Tsitsipas pia ameweka rekodi ya kuwa kijana mdogo
aliyetwaa taji katika fainali yake ya kwanza tangu John McEnroe alipofanya
hivyo mwaka 1978.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment