Meneja Uendeshaji Taasisi ya Vyuo Vikuu vya nje Tanzania 'University Abroad',
Rachel Mansuli, akizungumza na mmoja kati ya wanafunzi 15 waliokwenda nchini Chini kusomea masomo ya udaktari, Sarah Phiri, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Novemba 28, 2019.
Meneja Uendeshaji Taasisi ya Vyuo Vikuu vya nje Tanzania 'University Abroad',
Rachel Mansuli, akizungumza na mmoja kati ya wanafunzi 15 waliokwenda nchini Chini kusomea masomo ya udaktari, Sarah Phiri, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Novemba 28, 2019.
Wanafunzi wanaokwenda kusoma masomo mbalimbali nchini China wakipitia taarifa zao kabla ya kuanza safari yaoNovemba 28, 2019.
Na Mwandishi Wetu
MENEJA Uendeshaji Taasisi ya Vyuo Vikuu vya nje Tanzania 'University Abroad'
Rachel Mansuli amewataka wanafunzi wanaokwenda kusoma nje kuzingatia
kilichowapeleka ili waweze kurejea na ujuzi wa kulisaidia Taifa.
Ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga wanafunzi 15 walioelekea nchini China kwa ajili ya masomo katika kozi mbalimbali.
Rachel amesema kundi hilo la wanafunzi 15 kuna wanaokwenda kusomea Udaktari, Urubani pamoja na Uchumi na Biashara.
"Matarajio
yetu ni kuona vijana hawa wanakwenda kupata ujuzi ambao watarudi hapa
nyumbani kuja kushirikiana na wataalamu wengi ili kuweza kuisadiaa nchi
yetu kupiga hatua.
"Wamo
madaktari ambao tunaamini elimu wanayoenda kuipata itawapa uwezo wa kuja
kujenga taifa letu, vivyo hivyo kwa Wahandisi na Wachumi wa Biashara.
"Kikubwa
tunawasihi na kuwaomba wakafanye kinachowafanya kuziacha familia zao na
taifa lao ili baadae warejee kutoa mchango wao kwa nchi yetu".
Baadhi
ya Wanafunzi ambao wameondoka wametoa shukrani zao kwa taasisi hiyo na
familia zao kwa kuwawezesha kuanza safari ya kutimiza ndoto zao.
"Natambua
nchi yetu ina ombwe kubwa la wataaalamu wa Afya, hivyo basi mapenzi
yangu ya kuwa daktari ni sehemu ya kwenda kupata ujuzi ili nije kutoa
mchango wangu kwenye Taifa langu ". amesema Sara Phiri mwanafunzi wa
Udaktari.
"Nimechagua
kwenda kusoma nje ili nikapate ujuzi wa juu zaidi katika fani hii ya
Uinjinia kwani bado kama nchi tunahitaji wataaalamu wengi hasa katika
kuelekea Tanzania ya Viwanda "amesema Bernard Swara anenda kusomea
Uinjinia.
"Tunapenda
kutoa shukrani za dhati kwa University Abroad kuwa sehemu ya kufanikisha
safari ya kutimiza ndoto zetu ili tuweze kupata maarifa na ujuzi wa
kuja kurijenga Taifa letu ".amesema Everest Munish mwaanafunzi wa Uchumi
na Biashara.
Hii ni
awamu ya tano kwa University Abroad kupeleka wanafunzi katika mataifa
mbali mbali mwaka huu ambapo wanatarajia kuwa na awamu nyingine mbili
kabla ya mwaka kukamilika.
No comments:
Post a Comment