Na Tatu Mohamed
MWANAFUNZI
wa Chuo cha Mzumbe ambaye ni raia kutoka China Jianpo Zhang amesema
anajisikia fahari kuoa Tanzania akidai kufanya hivyo mbali na kudumisha
undugu baina ya familia hizo pia kunazidi kuboresha Uhusiano wa nchi za
Tanzania na China.
Katika
kuthibitisha kwa vitendo furaha aliyonayo Raia huyo wa China amefanya
sherehe kubwa ya kuwashukuru Watanzania na hasa wote ambao wameshiriki
kikamilifu katika kufanikisha ndoa yake na mkewe Shamsa Shaban Zhang.
Ndoa
hiyo ilifungwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi mstaafu Robert Mboma.
Akizungumza
wakati akitoa shukrani hizo Zhang amesema anajivunia kuoa mtanzania
huyo akisisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na kitendo chake cha
kufunga ndoa hiyo kitazidi kumfanya ajisikie kuwa kama yupo nyumbani
huku akiwataka watanzania kuona fahari pia kwenda kuoa raia kutoka
China.
Amesema katika
kipindi cha miaka mitatu aliyoishi nchini ameona mambo mengi mazuri na
kiasi cha kumfanya ajihisi yupo ‘nyumbani’ na zaidi akidai kuwa amani
na upendo kutoka kwa watanzania ndiyo hasa jambo linalozidi kumuongezea
hamasa ya kuona undugu unazidi kukua baina ya mataifa yote mawili.
Ameongeza
kuwa furaha kwake Tanzania inazidi kukua kimaendeleo siku hadi siku
chini ya uongozi wa Rais John Magufuli ambaye pia anasema katika
utawala wake ameona wazi wazi ushirikiano baina ya Tanzania na China
ukizidi kuhimarika.
“Naipenda
Tanzania, nawapenda watu wake na zaidi Rais John Magufuli ambaye katika
utawala wake naona mambo mengi mazuri ukiwemo ujenzi wa miradi
mbalimbali ikifanyika katika kiwango cha hali ya juu” amesema Zhang.
Amesema
mipango yake ya baadae ni kufanya biashara mbalimbali zinazoakisi
mahitaji muhimu ya kijamii ili ziweze kuzidi kumuweka karibu na
watanzania anaodai kuwa kwa sasa ni ndugu zake hasa baada ya kumuoa
Shamsa.
No comments:
Post a Comment